Loading...

MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA

Loading...
MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA
link : MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA

soma pia


MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA

NA TIGANYA VINCENT

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri amewaagiza Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kuhakikisha hakuna mtoto anayeanza Darasa la Kwanza bila kuwa amepitia darasa la Awali.

Hatua hiyo inalenga kuondoa tatizo la kuwa na wanafunzi wanaoingia Darasa la Kwanza ambao hawajui kusoma, kuhesabu na kuandika.

Mwanri alitoa kauli hiyo hivi wakati akifungua mkutano wa kutathmini masuala ya elimu mkoani humo na kuhimiza walimu kuhakikisha wanaondoka tatizo la KKK shuleni kwao.

“Msingi mzuri wa mtoto lazima uanzie elimu ya awali na ndio maana nasistiza kuwa mtoto asiingie la kwanza kama akupitia Chekechea …kule ndipo mtoto anapoandaliwa kuwa na maendeleo mazuri kitaaluma …ukikosea toka hapo basi mtoto anaweza kutokuwa na maendeleo mazuri darasani” alisema.

Alisema vitendo vya baadhi ya walimu kutozingatia hilo na kuchukua watoto ambao hawakupita elimu za awali ndiko kunakosababisha baadhi yao wanapofanya mitihani ya kujipama ya Darasa la Nne matokeo yao sio mazuri kwa sababu ya kuanza la kwanza hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu.

Aidha Mwanri aliwapongeza walimu wa Shule za Awali na msingi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwatengenezaea msingi mzuri watoto hao ili wanapoendelea na masomo yao waweze kufanya vizuri.

Katika hatua nyingine amewataka wamiliki na walimu wa Shule za Awali kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri kwa watoto hao ili wapende kwenda shule.

Alisema maeneo hayo lazima yawe na vivutio wa michezo mbalimbali ya watoto wadogo ili pamoja na kujifunza wawe na muda wa kucheza kama sehemu ya burudani na elimu kwao.

Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ametoa wito kwa wazazi na wadau wengine kuweka mazingira mazuri ambayo yatawavutia  walimu hasa wale ajira mpya kupenda kufanya kazi katika maeneo yao.

Alisema mazingira hayo ni pamoja na kuwawekea vivutio kama vile kuwapa maeneo ya kulima , nyumba za kuishi kama hakuna nyumba za shule na wakati mwingine kuwapa chakula cha kuanzia maisha.

Mwanri alisema kuna baadhi ya maeneo hapa nchini yamefanikiwa kielimu kutokana na wazazi kuweka vivutio ambavyo vimewafanya walimu wanaporipoti kutofikia kuhama katika shule walizopangiwa.

“Tujenge utamaduni wa kuweka motisha kwa walimu wetu…kwa mfano mnaposikia leo kuna mwalimu mpya anaripoti katika shule yetu , mnaweza kukusanyika na kumlaki ili ajiene kuwa amefika nyumbani na sio ugenini” alisema.


Hivyo makala MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA

yaani makala yote MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/mtoto-asipopitia-darasa-la-awali.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MTOTO ASIPOPITIA DARASA LA AWALI MARUFUKU KUINGIA DARASA LA KWANZA MKOANI TABORA"

Post a Comment

Loading...