Loading...
title : MWIJAGE: VIWANDA VIDOGO, BIASHARA NDOGO VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI, MAENDELEO, USTAWI WA NCHI
link : MWIJAGE: VIWANDA VIDOGO, BIASHARA NDOGO VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI, MAENDELEO, USTAWI WA NCHI
MWIJAGE: VIWANDA VIDOGO, BIASHARA NDOGO VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI, MAENDELEO, USTAWI WA NCHI
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema viwanda vidogo na vya kati vina mchango mkubwa katika uchumi, maendeleo na ustawi wa nchi yoyote, kwa kuwa vinatoa ajira kwa watu wengi ikilinganishwa na viwanda vikubwa hivyo havipashwi kubezwa kwa namna yoyote.
Mhe. Mwijage ameyasema hayo Oktoba 28, 2018 wakati akihitimisha Maonesho ya Viwanda Vidogo Kitaifa yaliyofanyika Kitaifa kwa mara ya kwanza katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu kuanzia Oktoba 23.
“ Najua kuna watu wanapenda kubeza lakini napenda niwaeleze nafasi ya viwanda na biashara ndogo katika uchumi, maendeleo na ustawi ya nchi yoyote, Sisi Tanzania tangu uhuru mpaka leo tuna viwanda 54,000, lakini asilimia 99 ni viwanda vidogo, vidogo sana na vya kati; sisi siyo kilema kwenye viwanda nchi zote zipo hivyo, viwanda vyenye tija na vinavyoajiri watu wengi ni viwanda vidogo, vidogo sana na vya kati” alisema Mwijage.
Amesema pamoja na viwanda vidogo na vidogo sana kuwa na tija katika uchumi wa nchi viwanda hivyo pia ni shule na vinaweza kumilikiwa kirahisi huku akisisitiza kuwa lengo la Serikali ni kujenga uchumi jumuishi ambao nji rahisi ya kuufikia ni kupitia uchumi wa viwanda.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO), Prof.Sylvester Mpanduji ametoa wito kwa Watanzania kuwa, ili waweze kushiriki katika Ujenzi wa Uchumi waViwanda hawana budi kuanza na viwanda vidogo ambavyo SIDO itakahakikisha vinakuwa endelevu.
Akizungumzia Maonesho ya Viwanda Vidogo Prof. Mpanduji amesema yamesaidia kuwaleta wajasiriamali pamoja kuonesha bidhaa zao na kubadilisha uzoefu katika teknolojia, usindikaji na masuala mengine yanayohusu bidhaa wanazozalisha kupitia viwanda vidogo na vya kati.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akimkabidhi nakala ya Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa huo Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage wakati wa Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani humo,kuanzia Oktoba 23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018(kulia) Balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Shahabi Issa Gada.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza na wajasiriamali mara baada ya kutembelea mabanda yao katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi,kuanzia Oktoba 23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akizungumza na baadhi ya viongozi wa World Vision na Halmashauri ya Wilaya ya Itilima alipotembelea banda lenye bidhaa za sabuni zinazozalishwa kupitiakiwanda kidogo kilichopo wilayani Itilima, katika Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi, kuanzia Oktoba 23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Mhe. Tano Mwera akiwasalimia wananchi wakati wa Kilele cha Maonesho ya Viwanda Vidogo (SIDO) yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi, kuanzia Oktoba 23 na kuhitimishwa Oktoba 28, 2018.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MWIJAGE: VIWANDA VIDOGO, BIASHARA NDOGO VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI, MAENDELEO, USTAWI WA NCHI
yaani makala yote MWIJAGE: VIWANDA VIDOGO, BIASHARA NDOGO VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI, MAENDELEO, USTAWI WA NCHI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MWIJAGE: VIWANDA VIDOGO, BIASHARA NDOGO VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI, MAENDELEO, USTAWI WA NCHI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/mwijage-viwanda-vidogo-biashara-ndogo.html
0 Response to "MWIJAGE: VIWANDA VIDOGO, BIASHARA NDOGO VINA MCHANGO MKUBWA KATIKA UCHUMI, MAENDELEO, USTAWI WA NCHI"
Post a Comment