Loading...
title : NAIBU WAZIRI ASEMA IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA
link : NAIBU WAZIRI ASEMA IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA
NAIBU WAZIRI ASEMA IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA
NA TIGANYA VINCENT
VITUO vya kulelea na kutunza watoto yatima na wale walioko kwenye mazingira hatarishi nchini vimetakiwa kuiga utaratibu wa Kituo cha Shirika Masista wa Upendo wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora wa kumwekea kila mtoto mdogo mlezi na mwangalazi wake wa karibu wakati wote ili kuwafanya wasijione wapweke.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza kwa ajili ya kuwapa sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
Alisema utaratibu unaotumiwa na Kituo hicho wa kumwakea mtoto mlezi na mwangalizi wake wa karibu ambaye siye Sista ni njia nzuri ya kuwasaidia watoto kutojiona kama yatima kwa kuwa wapweke na kuisi yule ndiye mzazi wake.
Aidha Naibu Waziri huyo alilipongeza Shirika hilo kwa malezi na huduma nzuri wanazotoa kwa watoto hao na wazee wasijiweza jambo ambalo limefanya waishi kwa furaha na ushirikiano miongoni mwao.
Alisema kazi inayofanywa na Shirika hilo ni nzuri na kubwa ambayo kimsingi ilikuwa ifanywe na Serikali lakini wao wameamua kwa upendo wao kuwalea na kuwatunza watoto ambao wamepoteza wazazi wao na wazee wasijiweza ambao wametelekezwa na ndugu zao.
Dkt. Ndumbalo aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutoa ushirikano kwa kadiri itakavyowezekana kwa Shirika hilo na mengine ambayo yanatunza watoto walioko katika mazingira hatarishi na wazee wasiojiweza ili nao wajione kuwa ni Watanzania sawa na wengine.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akisalimia wazee leomara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza kwa ajili ya kuwapa sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akimsalimia Mzee Lucas Simon(kushoto) leo mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza kwa ajili ya kuwapa sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
Kaimu Mama Mkuu wa Shirika la Masista wa Wamisionari wa Upendo wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Sisita Emmanuella MC (kushoto) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro(katikati) leo mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza kwa ajili ya kuwapa sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ na kuwakuta wakitumia utaratibu wa kila mtoto kuwa na mlezi wake.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Daniel Ndumbaro akikabidhi maziwa na sukari kwa Masisita mara baada ya kutembelea Kituo cha Shirika Masista wa Upendo la Jimbo Kuu Katoliki Tabora kinacholea watoto yatima na wale waliokuwa wakiishi katika mazingira magumu na wazee wasijiweza kwa ajili ya kuwapa sukari, maziwa ya watoto wachanga na ‘pampas’ leo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala NAIBU WAZIRI ASEMA IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA
yaani makala yote NAIBU WAZIRI ASEMA IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI ASEMA IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/naibu-waziri-asema-igeni-utaratibu-wa.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI ASEMA IGENI UTARATIBU WA KILA MTOTO KUWA NA MLEZI WAKE KATIKA VITUO VYA KULELEA WATOTO YATIMA"
Post a Comment