Loading...

NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR…

Loading...
NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR… - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR…, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR…
link : NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR…

soma pia


NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR…

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

KABLA yakuendelea naomba msomaji wangu alau kwa dakika moja fumba macho. Kisha wewe na mimi tumuombe Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za ndugu zetu 226 mahala pema peponi Amina.

Ni ndugu zetu  ambao wamepoteza uhai wao baada ya Kivuko cha MV. Nyerere kupinduka Septamba 20 mwaka huu katika Kisiwa cha Ukara mkoani Ukewere mkoani Mwanza. Ni moja ya ajali mbaya kuwahi kutokea ndani ya nchi yetu. Ni ajali ambayo sitaki hata kuisikia ikizungumzwa au kujadiliwa.

Ni ajali ambayo inasikitisha, inahuzunisha na inaumiza moyo. Huo ndio ukweli. Watanzania 226 kupoteza maisha kwa siku moja si jambo ambalo linaweza kusahaulika kwenye maisha yetu.

Waliopona katika ajali hiyo ni watu 41 tu. Inaumiza kwa kweli. Wakati naendelea kukusanya nguvu ili kueleza kile ambacho nimekikusudia naomba nitumie nafasi hiyo kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa namna ambavyo wameshughulikia tukio hilo.
Rais Magufuli pamoja na walio chini yake walihakikisha wanafuatilia hatua kwa hatua kuhusu ajali hiyo. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amezungumza mara kadhaa namna ambavyo alikuwa anapigiwa simu na Rais.

Kwa ujinga wangu na akili zangu fupi ambazo zinashindwa kuwaza mbali, baada ya kutokea ajali hiyo nikawa najiuliza maswali mengi lakini sikuwa na majibu yake. Sitaki kujiuliza tena maana najua sitaweza kujijibu mwenyewe. Acha nikae kimya huenda ninayojiuliza kuna watu wenye akili nyingi na maarifa nao wanajiuliza kama mimi. Lakini Najua watakuwa na majibu.
Kwa mfano swali la kwanza kujiuliza ndani ya Kivuko kulikuwa na watu wangapi? Nilijiuliza swali hili zaidi ya mara 100 sikuwa na majibu. Hata hivyo jibu nikajakulipata baadae kwamba idadi ya watu waliokuwa kwenye Kivuko hicho siku ya tukio walikuwa zaidi ya 265.

Baada ya kufahamu idadi ya watu...nikajiuliza tena wakati wanaingia walipita wapi? Walipita njia sahihi au? Wahusika wa Kivuko hicho wanajua idadi halisi ya waliokuwa wanatakiwa kubebwa na Kivuko? Kama walikuwa wanajua kwanini waliacha watu wote wakaingia?

Ulikuwa mpango maalum? Kwanini hawakuchukua tahadhari? Yaani najiuliza maswali mengi mengi mnooo… Ndio maana nasema acha nikae kimya tu. Najua ipo Tume ambayo imeundwa kuchunguza ajali ya MV.Nyerere.Hata hivyo kwa nafasi yangu ninayo nafasi ya kujadili kama ambavyo wengine wanajadili. Kwani kuna ubaya gani? Naomba niseme tu siingilii  Tume inayochunguza ajali hiyo maana sijui wao wanauliza maswali ya aina gani. Wakiuliza kama yangu nayo si tatizo.

Sitaki kuzungumza. Naomba niwe mkweli tayari tumeelezwa kuwa uwezo wa Kivuko cha MV. Nyerere ilikuwa ni kubeba watu 101. Hivyo siku ambayo Kivuko hicho kimepinduka kulikuwa na idadi ya watu zaidi ya 265. Najuliza kwanini iwe hivyo? Huenda nikawa na jibu langu acha nawe msomaji uwe na jibu lako.


Ukweli utabaki kuwa kivuko hicho kilibeba idadi ya watu tofauti na uwezo wake. Hiki ni chanzo namba moja cha Kivuko hicho kupinduka. Najua watalaam wanayo nafasi ya kufanya uchunguzi wao na kuja na majibu halisi ya kilichosababisha ajali.
Rais wangu Dkt. Magufuli wakati anazindua Flyover ya Mfugale iliyopo makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam amewaambia Watanzania kila mmoja kwa nafasi yake ajitafakari.

Nami kama Mtanzania nikaanza kuitafakari kauli ya Rais ya kututaka sote tujitafakari kuhusu ajali ya MV.Nyerere.Kuna somo la kujifunza kutokana na ajali ya MV. Nyerere. Hata hivyo swali la msingi la kujiuliza tumejifunza nini? Jibu la swali hili nadhani kila mmoja atakuwa na lake.

Kwangu mimi nilichojifunza kuna uzembe wa kusimamia Sheria, Kanuni na Taratibu kuhusu vivuko. Si vyote. Ni kwa hicho cha MV Nyerere. Sitaki ugomvi wala shari na mtu. Pia nimejifunza iko haja ya kuhakikisha Sheria, Kanuni na Taratibu zinaheshimiwa. Tukifuata sheria naamini tutakuwa salama na tutaepuka ajali.  Kwa kuwa kuna tume inachunguza acha hili nisiendelee kulizungumza. Tutafahamu ukweli wakati ukifika.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR…

yaani makala yote NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR… Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR… mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/najua-tuumejifunza-ajali-ya-mv-nyerere.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NAJUA TUUMEJIFUNZA AJALI YA MV NYERERE, SASA TUJADILI MWENDO KASI NA TRENI DAR…"

Post a Comment

Loading...