Loading...

RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE

Loading...
RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE
link : RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE

soma pia


RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE


 NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
30 OKTOBA 2018

SERIKALI  Mkoani Tabora imemtaka  mzabuni aliyeshinda na kusaini mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja kutoa huduma ya dawa na vifaa tiba (JAZIA- Prime Vendor System) kuhakikisha orodha ya dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba vilivyopo kwenye mkataba vinapatikana wakati wote ili kuepuka malalamiko kutoka kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora Msalika Makungu wakati wa hafla fupi ya kusaini mkataba na Kampuni ya Chacha Magasi Pharmacy Ltd na Serengeti Care  kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo ambazo hazipatikani Bohari Dawa(MSD). 

Katibu Tawala Mkoa alisema afya bora ni kitu muhimu sana ndio maana Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga fedha nyingi kwa ajili ya dawa na vifaa tiba ili kuwawezesha wananchi kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na kuongeza ndio maana hakuna sababu ya kutokuwepo dawa katika Kituo cha Afya chochote.

Aidha Makungu aliwataka Wakurugenzi Watendaji wote kuhakikisha wanasimamia makubaliano yaliyomo katika mkataba huo ikiwa ni pamoja na kuwahimiza wasimamizi wa vituo vya  kutolea huduma kuagiza dawa kutoka Bohari ya Dawa(MSD) na zile zitakazokosekana MSD ziagizwe kwa Mzabuni aliyeingia na Mkoa huo Mkataba na siyo vinginvyo.

Alisema ni vema waka wanafuatilia ili kuhakikisha Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali wakati wote zinakuwa na  dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba vya kutosha ili wagonjwa wasipate usumbufu.

Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba alisema lengo la JAZIA ni kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba katika Vituo vya kutolea huduma, kuboresha uwazi na uwajibikaji kwenye matumizi fedha za umma na kupunguza muda wa kuomba na kupokea dawa na vifaa tiba.

Baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya Mkoani Tabora wakiwa katika hafla fupi ya kusaini mkataba wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo jana. 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Gunini Kamba akitoa maelezo mafupi kuhusu uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo jana.
Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( mwenye suti ya bluu) akisaini Mkataba jana wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega Sekiete Yahaya naye akisaini huku wakishuhudiwa na Mkurugenzi wa Chacha Magasi Pharmacy Ltd  Chacha Magasi (wa pili kutoka kushoto)  na Serengeti Care Albinus Mongore(kushoto), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt Gunini Kamba(kulia aliyesimama)




5..Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu ( mwenye suti ya bluu waliokaa ) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote za Mkoa huo na watendaji wa Chacha Magasi Pharmacy Ltd   na Serengeti Care  mara baada ya kusaini Mkataba jana wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo. 



6,Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu akitoa maagizo jana  kwa Mzabuni aliyeshinda kutoa huduma kupitia unajulikana kama Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kuzingatia maelekezo ya mkabata kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo mara baada ya kusaini mkataba huo.



7.Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu (kulia ) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Nzega Philemon Magesa (kushoto) wakibadilishana mawazo mara baada ya kusaini mkataba jana wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo jana.



8.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Peter Onesmo Maloda  (kulia ) na Mwenyeikiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui) Said Ntahondi (kushoto) wakibadilishana mawazo mara baada ya kusaini mkataba jana wa uanzishwaji wa Mfumo wa Mzabuni Mmoja(JAZIA- Prime Vendor System) kwa ajili ya kukabiliana na ukosefu wa dawa, vitendanishi vya maabara na vifaa tiba katika Vituo vyote vya Serikali mkoani humo jana.






Picha na Tiganya Vincent
RS Tabora




Hivyo makala RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE

yaani makala yote RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/ras-tabora-aagiza-mzabuni-aliyeshinda_30.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "RAS TABORA AAGIZA MZABUNI ALIYESHINDA HUDUMA JAZIA KUHAKIKISHA DAWA ZILIZOPO KWENYE MKATABA ZIPATIKANA WAKATI WOTE"

Post a Comment

Loading...