Loading...

Rock City Marathon kufanyika kesho

Loading...
Rock City Marathon kufanyika kesho - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Rock City Marathon kufanyika kesho, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Rock City Marathon kufanyika kesho
link : Rock City Marathon kufanyika kesho

soma pia


Rock City Marathon kufanyika kesho

Mbio za Rock City Marathon msimu wa tisa zinatarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Maandalizi ya mbio hizo zinazotarajiwa kuanzia kwenye Daraja la Furahisha na kuishia kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini humo yamekamilika huku zaidi ya washiriki elfu tano (3,000) kutoka ndani na nje ya nchi wakitarajiwa kushiriki katika mbio hizo.

Tayari Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Dkt Philis Misheck Nyimbi wamekwisha thibitisha ushiriki wao kwenye mbio hizo ambazo pia zitahusisha ushiriki wa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali, wabunge na washiriki kutoka mashirika na taasisi mbalimbali.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Mwanza leo, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo Bw Zenno Ngowi alisema kamati yake imejiandaa kupokea washiriki zaidi ya 3,000 wa mbio hizo kutoka ndani na nje ya nchi wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa.

“Tunatarajia kuwa na mbio zenye mafanikio makubwa mwaka huu. Maandalizi kwa kiasi kikubwa yamekwisha kamilika na kinaochoendelea kwa sasa ni usajili wa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi na tunatarajia kufunga zoezi hilo siku ya Jumamosi Oktoba 27,’’ alibainisha.

Akizungumzia kuhusu zawadi, Ngowi alisema pamoja na medali washindi wa kwanza wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na wanawake watajinyakulia sh. Mil 4 kila mmoja, sh.mil 2/- kwa washindi wa pili na sh. Mil 1/- kwa washindi wa tatu, huku washindi wanne hadi kumi nao pia wakiibuka na medali na pesa taslimu.
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio  za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akionesha mbele ya waandishi wa habari baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo (kulia) na  Mwakilishi wa Kampuni ya Ulinzi ya KK Security ambao ni moja wa wadau wa usalama katika mbio hizo, Bw Andrew Maiga ndio
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio  za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akionesha mbele ya waandishi wa habari baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza. Wengine ni pamoja na Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo (kulia) na  Mwakilishi wa Kampuni ya Ulinzi ya KK Security ambao ni moja wa wadau wa usalama katika mbio hizo, Bw Andrew Maiga ndio
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mbio  za Rock City Marathon Bw Zenno Ngowi (katikati) akionesha baadhi ya zawadi zitakazotolewa kwa washindi wa mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho jijini Mwanza.
 Mratibu Mtaalamu wa mbio za Rock City Marathon Bw John Bayo akizungumza kuhusu maandalizi ya mbio hizo.



Hivyo makala Rock City Marathon kufanyika kesho

yaani makala yote Rock City Marathon kufanyika kesho Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Rock City Marathon kufanyika kesho mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/rock-city-marathon-kufanyika-kesho.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Rock City Marathon kufanyika kesho"

Post a Comment

Loading...