Loading...
title : Sekondari ya Zawadi yatimiza miaka kumi yalilia Umeme na Maktaba
link : Sekondari ya Zawadi yatimiza miaka kumi yalilia Umeme na Maktaba
Sekondari ya Zawadi yatimiza miaka kumi yalilia Umeme na Maktaba
Mwambawahabari
Na Heri Shaaban
SHULE ya Sekondari ya Zawadi iliyopo Tabata Wilayani Ilala imetimiza miaka kumi tangu kuanzishwa kwake huku ikikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Maktaba ,Umeme darasani hali inayopelekea wanafunzi kushindwa kujisomea vizuri.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam leo katika risala ya shule hiyo iliyosomwa na Jackline Mtei, wakati wa kutimiza miaka kumi ya shule hiyo iliyokwenda sambamba na mahafali ya kidato nne ya sekondari ya Zawadi.
"Shule yetu inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme katika vyumba vya madarasa,ukosefu wa maktaba,uchakavu wa sakafu madarasani hali inayopelekea kushindwa kusoma vizuri"alisema Mtei.
Mtei alisema changamoto zingine hawana projetor na screen ambazo zingesaidia ufundishwaji wa idadi kubwa wa wanafunzi na kuongeza ufaulu kwa kiwango cha juu zaidi.
Pia alisema changamoto zingine madarasa machache,hali inayopelekea kuwepo kwa msongamano darasani na kupunguza usikivu na ufaulu kwa wanafunzi .
Aliomba kwa mgeni rasmi Ofisa Elimu kata wawezeshwe kupatiwa viti na meza kwa Walimu na wanafunzi ,wajengewe maktaba na kumaliza uzio wa shule hiyo kwa usalama wa wanafunzi.
Aidha alisema walianza kidato cha kwanza 250, Jumla ya wahitimu 222 wakiwemo wasichana 106 na wavulana 116 wengine wameshindwa kutokana na sababu tofauti ikiwemo mimba,utoro,vifo na maradhi.
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya Zawadi Joyce Ngawilla alizungumzia mafanikio alisema kupanda kwa kiwango cha ufaulu kwa kidato cha nne na kidato cha pili imetokana na ushirikiano baina ya walimu,wanafunzi na Wazazi wa watoto wa shule hiyo.
Ngawila alisema mafanikio mengine wamejenga mahabara za Kisayansi ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kujifunza kwa vitendo pamoja na ufanyaji uchunguzi wa sayansi.
Pia wamesaidia kuwa na mafunzo na ujasiri kwa skauti ambao usaidia katika suala la ulinzi na usalama na taasisi ya Afrika Muslimu Agencey imechimba kisima cha maji yanayotumika katika shule hiyo.
Hivyo makala Sekondari ya Zawadi yatimiza miaka kumi yalilia Umeme na Maktaba
yaani makala yote Sekondari ya Zawadi yatimiza miaka kumi yalilia Umeme na Maktaba Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Sekondari ya Zawadi yatimiza miaka kumi yalilia Umeme na Maktaba mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/sekondari-ya-zawadi-yatimiza-miaka-kumi.html
0 Response to "Sekondari ya Zawadi yatimiza miaka kumi yalilia Umeme na Maktaba"
Post a Comment