Loading...

SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI

Loading...
SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI
link : SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI

soma pia


SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI

Naibu Waziri Dkt.Faustine Ndugulile akikagua madaftari ya wagonjwa waliolazwa wodi ya akina mama kwenye hospitali ya Wilaya ya Manyoni,kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi.Rahabu Solomon

NA WAMJW-MANYONI

Serikali imetangaza neema ya kupeleka gari ya  wagonjwa (Ambulance)  katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni ili kutatua tatizo linaloikabidi Wilaya hiyo hususan ya vifo vitokanavyo na uzazi.

Ahadi hiyo imetolewa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipoitembelea hospitali hiyo kwa lengo la kutazama utoaji wa huduma za afya ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tatu katika mkoa wa Singida.

Dkt. Ndugulile amefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza kero kutoka kwa wananchi wanaotumia hospitali hiyo ambapo wengi walisema kungekuwepo na gari ya wagonjwa kungeepusha vifo vya akina mama wajawazito na watoto pamoja na wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura.

"Naomba niwaahidi wananchi wa Manyoni, Serikali imeagiza magari ya kubebea wagonjwa ambayk yanaweza kufika mwezi Disemba mwaka huu,hivyo nitahakikisha katika mgao wa magari hayo basi na hospitali hii ya Wilaya  inapata gari moja kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi wa hapa. Alisema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Dkt.Ndugulile aliahidi kuwatafutia wataalam wa Afya watakaoweza kwenda  kupunguza uhaba wa watumishi wanaokabiliana nayo hospitali hiyo

Naye Mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Atupele Mohamed alisema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa majengo ikiwemo chumba cha huduma za uzazi ambapo uwezo wake kwa mwezi ni  kuzalisha akina mama 90 lakini kwa sasa huzalisha  wastani wa akina mama 400.

Aidha, Dkt. Atupele alisema Hospitali hiyo ina upungufu mkubwa wa watumishi wenye sifa, ambapo ina jumla ya watumishi 107 sawa na asilimia 53 ya watumishi wanaohitajika.

Dkt. Atupele alitaja   uhaba mkubwa wa watumishi hao  ni Madaktari, Wauguzi, Wataalamu wa mionzi na wataalamu wa kutoa huduma za usingizi.

Katika Wilaya hiyo Naibu Waziri huyo aliweza kutembelea  kutembelea kituo cha kulea wazee na wasiojiweza cha Sukamahela pamoja na Hospitali ya rufaa ya Mtakatifu Gasper iliyopo  Itigi na  kuridhika na hali ya utoaji wa huduma za afya katika Hospitali hiyo.



Hivyo makala SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI

yaani makala yote SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/serikali-yaahidi-kupeleka-gari-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YAAHIDI KUPELEKA GARI YA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA MANYONI"

Post a Comment

Loading...