Loading...
title : TAMASHA KUBWA LA MADINI KUTIMIZA MIAKA 50 YA UGUNDUZI WA TANZANITE KUFANYIKA DEC 6-8
link : TAMASHA KUBWA LA MADINI KUTIMIZA MIAKA 50 YA UGUNDUZI WA TANZANITE KUFANYIKA DEC 6-8
TAMASHA KUBWA LA MADINI KUTIMIZA MIAKA 50 YA UGUNDUZI WA TANZANITE KUFANYIKA DEC 6-8
Taasisi ya mfuko wa mgunduzi wa madini ya Tanzanite inatarajia kufanya Tamasha na maonyesho ya madini ya Tanzanite lengo likiwa ni kumuenzi mgunduzi wa madini hayo Mzee Jumanne Ngoma.
Hayo yameelezwa na mwenyekiti mtendaji wa Taasisi hiyo Bi Asha Ngoma alipokuwa akiongea na wadau wa sekta ya madini mkoani hapa na kueleza kuwa katika tamasha hilo watashiriki kuonyesha zana mbalimbali alizokuwa akitumia mgunduzi huyo pamoja na madini aliyowahi kupata.
Amesema kuwa lengo la kikao kuongea na wadau kuhusu uandaaji wa tamasha la madini hayo ambapo maonyesho hayo kutangaza nchi ili madini hayo yajulikane yanatoka hapa nchini kwani sekta hiyo na wadau wake watanufaika kutokana na maonyesho hayo.
“Tunaenda kukutana na Serikali kwani wadau wamefurahia kuaandaa tamasha hili kutimiza miaka 50 tokea kugunduliwa kwa madini ya tanzanite na maonyesho hayo yatafanyika mwezi wa 12 tarehe 6-8 mwaka huu”alisema Ngoma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa madini na vito hapa nchini(Tamida) Sammy Mollel alisema kuwa tamasha hilo limekuja wakati muafaka na kuunga mkono uwepo wa tamasha hilo kwani litasaidia ukuaji wa kiuchumi na udhibiti wa madini ya Tanzanite ambapo madini haya yanatoka hapa nchini pekee amhali yalipogunduliwa madini hayo.
Amesema kuwa kutakuwa na maonyesho ya uzaji na ununuzi wa madini ya vito na pia kutembelea sehemu ambayo yaligunduliwa madini hayo ambapo tunatarajia kujenga mnara wa kuenzi ugunduzi wa madini hayo eneo hilo na tunaendelea kumpongeza mh.Rais kwa kujenga ukuta ambao unadhibiti madini hayo.

Alieleza jusikitishwa kwake na wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hayo kumsahau mgunduzi hiyo Mzee jumanne ngoma kwa mchango wake kwani alitumia uwezo na rasilimali zake katika kugundua madini hayo ambayo yameweza kuwatajirisha watu wengi ilhali yeye akibakia maskini.
“Naipongeza Taasisi hii ya mgunduzi wa madini ya Tanzanite kwa uamuzi wao wa kuaandaa tamasha hilo ambalo litakuwa na maslahi mapana kwa taifa na wadau wa sekta ya madini ya vito nchini napenda kuishauri tamasha hilo likafanyika eneo la merelani ndani ya ukuta au nje ya ukuta lengo ni serikali kupata mapato yake”alisisitiza Munisi
Hivyo makala TAMASHA KUBWA LA MADINI KUTIMIZA MIAKA 50 YA UGUNDUZI WA TANZANITE KUFANYIKA DEC 6-8
yaani makala yote TAMASHA KUBWA LA MADINI KUTIMIZA MIAKA 50 YA UGUNDUZI WA TANZANITE KUFANYIKA DEC 6-8 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAMASHA KUBWA LA MADINI KUTIMIZA MIAKA 50 YA UGUNDUZI WA TANZANITE KUFANYIKA DEC 6-8 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/tamasha-kubwa-la-madini-kutimiza-miaka.html
0 Response to "TAMASHA KUBWA LA MADINI KUTIMIZA MIAKA 50 YA UGUNDUZI WA TANZANITE KUFANYIKA DEC 6-8"
Post a Comment