Loading...
title : RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA "FLYOVER" YA MFUGALE, TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM
link : RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA "FLYOVER" YA MFUGALE, TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM
RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA "FLYOVER" YA MFUGALE, TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuutaarifu Umma kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za ufunguzi wa Flyover ya Mfugale katika makutano ya barabara za Mandela na Nyerere eneo la TAZARA tarehe 27 Septemba, 2018 jijini Dar es Salaam.
Ujenzi wa Flyover ya Mfugale ulianza tarehe 15 Oktoba, 2015 ambapo jiwe la msingi liliwekwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 16 Aprili, 2016.
Flyover ya Mfugale inajumuisha barabara mbili za juu; moja kutoka Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere kuelekea katikati ya jiji na nyingine kutoka katikati ya jiji kuelekea Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Kukamilika kwa Flyover ya Mfugale kutapunguza msongamano wa magari katika eneo la TAZARA na kupunguza muda wa safari toka katikati ya jiji kwenda Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa wa Julius Nyerere na kurudi, na pia kurahisisha usafiri na usafirishaji kwa watumiaji wa barabara za Mandela na Nyerere.
Wananchi wote mnakaribishwa katika ufunguzi huo.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
26 Septemba, 2018.
Hivyo makala RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA "FLYOVER" YA MFUGALE, TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM
yaani makala yote RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA "FLYOVER" YA MFUGALE, TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA "FLYOVER" YA MFUGALE, TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/09/rais-dkt-magufuli-kufungua-flyover-ya.html
0 Response to "RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA "FLYOVER" YA MFUGALE, TAZARA JIJINI DAR ES SALAAM"
Post a Comment