Loading...

TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI

Loading...
TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI
link : TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI

soma pia


TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimejipanga kuzuia na kudhibiti madhara yanayosababishwa na machafuko ya kisiasa katika jumuiya hiyo na Bara la Afrika kwa ujumla. Wawakilishi wa nchi hizo wamekusanyika nchini Malawi kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 17 Oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko

Wawakilishi wa Tanzania kutoka Jeshi la Wananchi, Magereza na taasisi za kiraia ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa watu 600 wanaoshiriki zoezi hilo lililopewa jina la EX UMODZI CPX 2018 na kaulimbiu ya Afrika ni Amani na Maendeleo (Africa for peace and prosperity).

Katika hafla ya ufunguzi wa mazoezi hayo iliyofanyika leo tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo mji wa Salima takriban kilomita 120 kutoka Lilongwe, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi, Mhe. Evaton Chemulirenji alisema mazoezi hayo ni utekelezaji wa maazimio ya SADC na Umoja wa Afrika (AU) wa kuandaa kikosi cha kukabiliana na machafuko barani Afrika (Standby Force-SF) ambacho kinatakiwa kiwe kimekamilika ifikapo Januari 2019.

Naibu Waziri wa Wizara ya Ulinzi wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Evaton Chimulirenji akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa mafunzo na mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko iliyofanyika tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo katika mji wa Salima nje kidogo ya jiji la Lilongwe.Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Sekretarieti ya SADC yanajumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na majeshi ya ulinzi, askari polisi, askari magereza na raia wa fani tofauti kama vile za Utawala wa Sheria, siasa, mawasiliano, Utawala, haki za binadamu na jinsia ambao wana mchango mkubwa katila masuala ya operesheni za kulinda amani.

Mratibu wa Program ya Mafunzo yanayofanyika nchini Malawi akieleza mpangilio wa program ya mafunzo hayo kwa ujumla

Mratibu Mkuu wa Mafunzo hayo Meja Jenerali A.B Mhone naye akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo

Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi Mhe. Evaton Chimulirenji (kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Malawi Generali Supini Phiri (kulia) pamoja na Mkuu wa Misheni ya mafunzo hayo, Mhe. Bi. Eunice Lumbia

Sehemu ya viongozi wa kijeshi wakifuatilia hotuba zilizokuwa zinatolewa wakati wa ufunguzi huo .

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>


Hivyo makala TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI

yaani makala yote TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/tanzania-kushiriki-mazoezi-ya-kikosi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TANZANIA KUSHIRIKI MAZOEZI YA KIKOSI CHA DHARURA CHA ULINZI WA AMANI CHA SADC NCHINI MALAWI"

Post a Comment

Loading...