Loading...
title : TCRA YAWATIA KIBANONI WANANE WANAODAIWA KUKIUKA SHERIA ZA MTANDAO KUANZIA JULY -SEPT
link : TCRA YAWATIA KIBANONI WANANE WANAODAIWA KUKIUKA SHERIA ZA MTANDAO KUANZIA JULY -SEPT
TCRA YAWATIA KIBANONI WANANE WANAODAIWA KUKIUKA SHERIA ZA MTANDAO KUANZIA JULY -SEPT
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeshawachukulia hatua za kisheria watu nane wanaodaiwa kukiuka sheria za mtandao, ikiwemo kusambaza picha za nusu uchi, video za ngono na kutupia matusi katika kipindi cha Julai -Septemba mwaka huu.
Aidha jamii imekemea matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na video za ngono kwani kwa kufanya hivyo hawatamuangalia mtu kwa sura ama umaarufu bali sheria itachukua mkondo wake.
Ofisa mkuu wa mawasiliano kwa umma (TCRA) Semu Mwakyanjala aliwatahadharisha ,watu wasisambaze picha ama video za ngono na kuanzisha tovuti hizo kwani ni kukiuka sheria .
Alieleza kuna faida unapotumia mtandao inarahisisha mawasiliano ,unapunguza gharama ,inaokoa muda ,inatoa elimu na kukuza biashara badala ya kutumia masuala yasiyo na tija.“Kwasasa hatuna masihala, tunashirikiana na jeshi la polisi kubaini wale wanaokaidi kufuata sheria zilizopo “alieleza Mwakyanjala. Aliiomba jamii kutunza vifaa vya kielektronik ili watu waeiibe na kutymia vibaya .
Nae mkuu wa kanda ya Mashariki (TCRA) Lawi Odiero alisema, sheria ya kielektroniki iliyopo inakataza kusambaza ngono na baadhi ya watu wanachukuliwa hatua ya kulipa faini sh. mil tano ama miaka mitatu jela.
Aliwaasa wananchi kwenda kutembelea banda lao kujifunza ili kuelewa sheria zinazowabana ili kuepukana na adhabu. Odiero alieleza wazingatie wasiweke namba za siri kwenye simu ama internet miaka ya kuzaliwa bali watumie maneno mengine kwani sio rahisi kughushi .Akizungumzia ving’amuzi alisema ,serikali kupitia TCRA iliondoa baadhi ya channel kwenye baadhi ya visimbuzi.
Odiero alifafanua, Azam, Dstv na Zuku huduma wanatoa kwa kulipisha hivyo hawaruhusiwi kubeba channel za ndani. Watumiaji wa internet hadi sasa nchini wapo milioni 22 ,luninga zipo 34 ,vituo vya redio zaidi ya 150 kutoka kituo kimoja kilichokuwepo mwaka 1961.
Hivyo makala TCRA YAWATIA KIBANONI WANANE WANAODAIWA KUKIUKA SHERIA ZA MTANDAO KUANZIA JULY -SEPT
yaani makala yote TCRA YAWATIA KIBANONI WANANE WANAODAIWA KUKIUKA SHERIA ZA MTANDAO KUANZIA JULY -SEPT Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TCRA YAWATIA KIBANONI WANANE WANAODAIWA KUKIUKA SHERIA ZA MTANDAO KUANZIA JULY -SEPT mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/tcra-yawatia-kibanoni-wanane-wanaodaiwa.html
0 Response to "TCRA YAWATIA KIBANONI WANANE WANAODAIWA KUKIUKA SHERIA ZA MTANDAO KUANZIA JULY -SEPT"
Post a Comment