Loading...
title : TRA yachangia Milioni 25 ujenzi wa maabara ya Kompyuta Misitu Sekondari
link : TRA yachangia Milioni 25 ujenzi wa maabara ya Kompyuta Misitu Sekondari
TRA yachangia Milioni 25 ujenzi wa maabara ya Kompyuta Misitu Sekondari
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imechangia kiasi cha Shilingi Milioni 25 kwa ajili ya ujenzi wa maabara ya Kompyuta katika shule ya Sekondari Misitu iliyopo Wilaya ya Ilala, jijini Da es Salaam.
Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere, ametoa mchango huo ikiwa ni sehemu ya kuchangia maendeleo kwa jamii alipokuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 9 ya kidato cha Nne katika shule hiyo ambapo wanafunzi 205 wanaotarajia kuhitimu masomo yao mara baada ya kufanya mtihani wa Taifa mwezi Novemba 2018.
Kamishna Mkuu Bw. Kichere, amesema kuwa kiasi hicho cha fedha kitachangia ujenzi wa Maabara ya Kompyuta na kuwafanya wanafunzi kujifunza na kuongeza uelewa zaidi wa masuala ya Teknolojia.
“Nimesikia katika changamoto mlizozitaja kuwa mnahitaji jengo la maabara ya kompyuta, uzio pamoja na jengo la utawala na mimi nimeona vyema nichangie ujenzi wa jengo hilo ili wanafunzi wapate kujifunza na kuwa na uelewa wa teknolojia kwani dunia sasa inatumia zaidi teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuleta maendeleo”, alisema Kichere
Aidha, Bw. Kichere aliongeza kuwa, ujenzi na maendeleo ya shule za serikali unatokana na kodi hivyo aliwataka wanafunzi, walimu na wazazi kuwa na utamaduni wa kudai risiti za mashine za kielektroniki (EFD) ili kuchangia Mapato yatakayotumika kuboresha ujenzi na uboreshaji wa shule pamoja na shughuli mbalimbali za kijamii.
Bw. Kichere alisisitiza kuwa matunda ya kodi zinazopatikana pia hutumika kuboresha huduma mbalimbali za jamii kama vile ununuzi wa vitabu kwa ajili ya maktaba, utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, ujenzi wa madarasa, mabweni, nyumba za walimu na ununuzi wa vifaa vya maabara na kufundishia.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (mwenye skafu) akimkabidhi cheti mwanafunzi bora katika masomo yote wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam, Richard Sagwe wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere akiwahutubia Wanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (mwenye skafu) akiangalia baadhi ya kazi mbalimbali za Sanaa zinazofanywa na Wanafunzi katika shule ya sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Charles Kichere (mwenye skafu) akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Bw. Richard Kayombo (kushoto) pamoja na uongozi wa shule ya sekondari Misitu iliyopo Kivule Jijini Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya kidato cha nne shuleni hapo.
(PICHA ZOTE NA TRA)KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala TRA yachangia Milioni 25 ujenzi wa maabara ya Kompyuta Misitu Sekondari
yaani makala yote TRA yachangia Milioni 25 ujenzi wa maabara ya Kompyuta Misitu Sekondari Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TRA yachangia Milioni 25 ujenzi wa maabara ya Kompyuta Misitu Sekondari mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/tra-yachangia-milioni-25-ujenzi-wa.html
0 Response to "TRA yachangia Milioni 25 ujenzi wa maabara ya Kompyuta Misitu Sekondari"
Post a Comment