Loading...
title : WAKILI AIMBIA MAHAKAMA HANSPOPE ALIKUWA NCHINI MAREKANI KWA MATIBABU
link : WAKILI AIMBIA MAHAKAMA HANSPOPE ALIKUWA NCHINI MAREKANI KWA MATIBABU
WAKILI AIMBIA MAHAKAMA HANSPOPE ALIKUWA NCHINI MAREKANI KWA MATIBABU
Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WAKILI Augustine Shio anayemtetea Hanspope ameieleza Mahakama kuwa, Haspope alikuwa yupo nchini Marekani
Ameyaeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati akimuombea dhamana mteja wake.
Wakili Shio ameeleza kuwa Hanspope alikuwa nchini Marekani kwa matibabu lakini aliamua kukatisha matibabu hayo na kurudi nchini kusikiliza tuhuma zinazomkabili.
Amedai kuwa Hanspope alimuandikia barua na kumjulisha kuwa anarudi nchini Oktoba 15 mwaka 2018 na kumtaka awajulishe Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu ujio wake.
Wakili Shio amedai, aliwafikishia ujumbe Takukuru ndipo usiku wa jana Oktoba 15 2018, saa 7:25 usiku Hanspope aliwasili na alipofika Airport alikamatwa na Takukuru lakini baadaye waliweza kumruhusu alale nyumbani kwake na asubuhi walimfikisha mahakamani.
Hanspope kwa sasa yupo nje kwa dhamana, huku wenzake wawili ambao ni Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange wanaendelea kusota mahabusu.

Mtuhumiwa Haspope akitoka nje ya mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabiri.
Hivyo makala WAKILI AIMBIA MAHAKAMA HANSPOPE ALIKUWA NCHINI MAREKANI KWA MATIBABU
yaani makala yote WAKILI AIMBIA MAHAKAMA HANSPOPE ALIKUWA NCHINI MAREKANI KWA MATIBABU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKILI AIMBIA MAHAKAMA HANSPOPE ALIKUWA NCHINI MAREKANI KWA MATIBABU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wakili-aimbia-mahakama-hanspope-alikuwa.html
0 Response to "WAKILI AIMBIA MAHAKAMA HANSPOPE ALIKUWA NCHINI MAREKANI KWA MATIBABU"
Post a Comment