Loading...
title : WANAFUNZI 400 KUNUFAIKA NA ELIMU YA KUPINGA UKEKETAJI, ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
link : WANAFUNZI 400 KUNUFAIKA NA ELIMU YA KUPINGA UKEKETAJI, ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
WANAFUNZI 400 KUNUFAIKA NA ELIMU YA KUPINGA UKEKETAJI, ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Na Frankius Cleophace, Serengeti.
Wasichana zaidi ya 400 (Mianne) wa shule za sekondari wilayani Serengeti Mkoani Mara wamepatiwa elimu ya kupinga Ukeketaji kwa mtoto wa kike pamoja na elimu ya Afya ya Uzazi na utunzaji wa Mazingira kwa lengo la kukomboa Mwanamke huku wengine 1160 wakitarajia kupatiwa elimu hiyo. Hayo yamebainishwa na Frida Mollel ambaye ni Meneja Idara ya Maendekeo ya jamii kampuni ya Singita Grumeti Fund iliyopo wilayani Serengeti Mkoani Mara katika viwanja shule ya Msingi Makundusi baada ya kutoka Shule ya Msingi Natta kwa kukikbia mbio fupi.
Frida amesema kuwa wao kama kampuni wamekuwa wakitoa elimu mbalimbali kwa wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari na wanakijiji kutoka vijiji 21 vinavyozunguka hifadhi ya Ikorongo Grumeti Reserves ili kuendelea kutunza mazingira na jamii kuondokana na ujangiri ili kulinda hifadhi pamoja na wanyama ili kunufaisha kizazi kijacho.
Meneja Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Mollel akitoa elimu ya kupinga Ukeketaji na mila kandamizi kwa wasichana pamoja na wanawake katika viwanja vya shule ya Msingi Natta wilayani Serengeti mkoani Mara.
Licha ya kutolewa kwa elimu ya kutunza mazingira Frida amesema kuwa wanafunzi hao wamepewa elimu ya kupinga suala zima la ukeketaji na mila kandamizi ambazo zinazidi kundamiza mwanamke pamoja na msichana mpaka kushindwa kutimiza ndo zake ambapo elimu hiyo imeanza kutolewa tangu mwaka jana lengo ni kukomboa mwanamke.
“Mwaka jana tuliweza kukutana na wasichana wakatupa changamoto zinazowakumba kipindi cha ukeketaji na mwaka huu Serengeti kulingana na mila na desturi watakeketa sasa tumeona tutumie fursa hii kutoa elimu ili kukomboa mtoto wa kike ukiangalia pia kuna wanawake ambao wametoka nje ya nchi ya Tanzania kwa maana ya Afirika kusini na Marekani ili kutuunga mkono lengo ni kutoa hamasa kubwa kwa mabinti hao pia wameweza kukimbia mbio fupi ni wasichana hao alisema Frida.” alisema Frida.
Rnonda Vetere Kutoka New York City Marekani akiongea na wanafunzi wa shule za sekondari kuhusu mwanamke kijiamini ambapo amewasihi kudhubutu na kujiamini kwa lengo la kufanikiwa huku wakiendelea kutoa elimu juu ya kupinga mila kandamizi.
Katika kutoa elimu hiyo na kutoa hamasa kwa mabinti hao baadhi ya washiriki ambao wamekuwa wakitoa elimu wametoka nje ya Nchi huku baadhi yao wakitoka Afrika Kusini, na Marekani Rnonda Vetere kutoka New york City Nchini Marekani amezidi kuhamasisha wanawake Nchini Tanzaniakuendelea kujiamini na kudhubutu kwa lengo la kupata mafanikio ili kuendeleza mapinduzi katika kutokomeza Mila kandamizao ukiwemo Ukeketaji kwa mtoto wa kike.
Hivyo makala WANAFUNZI 400 KUNUFAIKA NA ELIMU YA KUPINGA UKEKETAJI, ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
yaani makala yote WANAFUNZI 400 KUNUFAIKA NA ELIMU YA KUPINGA UKEKETAJI, ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WANAFUNZI 400 KUNUFAIKA NA ELIMU YA KUPINGA UKEKETAJI, ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wanafunzi-400-kunufaika-na-elimu-ya.html
0 Response to "WANAFUNZI 400 KUNUFAIKA NA ELIMU YA KUPINGA UKEKETAJI, ELIMU YA AFYA YA UZAZI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA"
Post a Comment