Loading...
title : WASAFIRISHA MIZIGO MATATANI UKWEPAJI KODI.
link : WASAFIRISHA MIZIGO MATATANI UKWEPAJI KODI.
WASAFIRISHA MIZIGO MATATANI UKWEPAJI KODI.
Picha ya mashine kutolea risiti za Kielektroniki EFD.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kikodi Kariakoo Warioba Kanire akifanya ukaguzi wa matumizi ya mashine za kutolea risiti EFD katika maduka mbalimbali kariakoo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyabiashara wa Kariakoo wanaosafirisha mzigo kwenda mikoa mbalimbali wamejikuta wakiwa katika wakati mgumu baada ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwabaini hawafati utaratibu ikiwemo kutotumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti EFD wakati wateja wakifanya malipo.
Hatua hiyo imekuja baada jana (Oktoba 28 mwaka huu) majira ya saa I2 jioni TRA, Mkoa wa Kikodi Kariakoo kuendelea na oparesheni ya kuwatafuta wafanyabiashara wanaokwepa kodi, na kufanikiwa kuvikuta vituo viwili vya kusafirisha mizigo kwenda mikoa mbalimbali wakiendelea na shuguli zao bila kufata sheria na kanuni.
Akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika Oparesheni hiyo jijini Dar es Salaam Meneja wa TRA, Mkoa wa Kikodi Kariakoo Warioba Kanire, amesema kuna wafanyabiashara wa kusafirisha mizigo ambao sio waminifu wamekuwa na tabia ya kutotumia mashine kutolea risiti za Kielektroniki EFD kwa lengo la kuibia serikali kodi yake.
Kanire amesema kuwa katika mtaa wa muhonda kariakoo wamekuta kituo cha kusafirisha mizigo kinachodaiwa kumilikiwa na Emmanuel Mvanda wakiendelea na majukumu yao pasipo kutumia mashine ya EFD jambo ambalo wamekuwa wakiikosha serikali mapato.
"Wanatumia kitabu cha kawaida cha kutolea risiti ambacho kina TIN namba I34-222-689, na mfanyabiashara usipotoa risiti ya EFD ni sawa na kufanya malipo bila kutoa risiti kitu ambacho ni kinyume na utaratibu" amesema Kanire.
Katika hatua nyengine Kanire amesema kuwa mtaa wa masasi katika kituo cha kusafirisha mizigo cha Arusha United Cargo, wamekamata mizigo iliyokuwa ikita kusafirishwa kwenda mikoa ya kusini ambayo haina risiti za EFD zinazoonyesha gharama za manunuzi.
Amesema kuwa baada ya kuendelea kufanya ukaguzi katika kituo hicho wakabaini baadhi ya risiti zimeandikwa kiasi kidogo cha fedha tofauti na bei husika iliyopaswa kuandikwa.
"Hapa tumekuta hakuna mashine za EFD, na pia tayari tumekamata mizigo yote ambayo haina risiti lengo letu tuendelee kufanya uchuguzi ili tubaini mizigo hii wameitoa wapi" amesema Kanire.
Amesema kuwa mfanyabiashara yoyote atakayebainika hatumii risiti ya EFD atapigwa faini kuanzia milioni 3 na kuendelea pamoja na kupewa maelekezo ya kununua mashine ya kutolea risiti ya Kielektroniki ili kodi ya serikali ipatikane kwa ajili ya kufanikisha maendeleo ya Taifa.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mkoa wa Kikodi Kariakoo imekuwa ikifanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kila mfanyabiashara analipa kodi, huku wale wanaobainika wanaokwenda kinyume na utaratibu wanachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupigwa faini.
Hivyo makala WASAFIRISHA MIZIGO MATATANI UKWEPAJI KODI.
yaani makala yote WASAFIRISHA MIZIGO MATATANI UKWEPAJI KODI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WASAFIRISHA MIZIGO MATATANI UKWEPAJI KODI. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wasafirisha-mizigo-matatani-ukwepaji.html
0 Response to "WASAFIRISHA MIZIGO MATATANI UKWEPAJI KODI."
Post a Comment