Loading...

WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA.

Loading...
WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA.
link : WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA.

soma pia


WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA.


Na Mwandishi Wetu Manyoni Singida

Wazee na wasiojiweza waishio katika Makao ya Wazee Sukamahela yaliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida wamelalamika kupata aina moja ya chakula kwa muda mrefu.

Hayo yamesemwa na baadhi ya Wazee hao walipokuwa wakitoa malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile alipotembela kujionea Huduma zinazotokewa katika Makazi ya Wazee na Wasiojiweza ya Sukamahela.

Wazee hao wamesema wamekuwa wakipata hasa aina moja ya mboga aina ya maharagwe kwa mlo wa mchana na usiku kwa siku zote za wiki.

Akijibu changamoto hizo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali inahudumia Wazee na Wasiojiweza katika Makao 17 nchini na inaendelea kutoa huduma stahiki kwa Wazee hao.

Dkt. Ndugulile amemuagiza  Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi kupeleka fedha kwa wakati katika Makao ya Wazee na Wasiojiweza nchini ili kuondokana na changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza.

Pia Naibu Waziri Ndugulile pia amemuagiza  Afisa Ustawi Mfawidhi wa Makao ya Wazee na Wasiojiweza ya Sukamahela kuandaa ratiba ya chakula stahiki kwa ajili ya wahudumiwa na kuibandika katika eneo la wazi.

"Niseme kuwa fedha zipo za kuwahudumia Wazee na Wasiojiweza katika Makao ya Wazee na Wasiojiweza nchini watendaji timizeni wajibu wenu katika kuhudumia kundi hili" Alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Akisoma taarifa ya Makao ya Wazee na Wasiojiweza ya Sukamahela Afisa Ustawi Mfawidhi wa Makao hayo Bw.  Mgoo Senge amesema Makao hayo yanakabiriwa na uchakavu wa majengo pamoja na kukosa ulinzi kutokana na kutokuwa na uzio katika eneo hilo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile yupo mkoani Singida kwa ziara ya siku mbili kukagua shughuli za Sekta ya Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jami


Hivyo makala WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA.

yaani makala yote WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/wazee-sukamahela-walalamikia-aina-moja.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZEE SUKAMAHELA WALALAMIKIA AINA MOJA YA CHAKULA."

Post a Comment

Loading...