Loading...

WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA

Loading...
WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA
link : WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA

soma pia


WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA

IMEELEZWA kuwa kukamilika mapema kwa barabara za lami na madaraja ya kisasa katika mkoa wa Ruvuma kutauunganisha kirahisi na mikoa ya nyanda za juu kusini na nchi za jirani na hivyo kuhuisha uchumi wa wakazi wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe amesema hayo alipokagua ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 60 na kumtaka mkandarasi china Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO), anayejenga barabara hiyo kuikamilisha kwa wakati.
Amesema fursa za kilimo, uvuvi, usafirishaji na uchukuzi wa mazao na makaa ya mawe katika mkoa wa Ruvuma zinahitaji barabara za lami na zenye uwezo wa kupitika wakati wote na kwa urahisi hivyo kukamilika kwa barabara za lami kwa wakati kutaleta ukombozi kwa wananchi wa mkoa huo.
“Viwanda vingi sasa vinatumia makaa ya mawe tena kwa kiwango kikubwa hivyo tunahakikisha usafiri katika mkoa huu unakuwa wa uhakika ili kuufungua na kuunganisha na mikoa mingine kwa njia fupi  na  hivyo kuongeza biashara ya ndani kuvutia biashara na nchi za jirani”, amesema Mhandisi Kamwelwe.
Amesisitiza kuwa  Serikali imejipanga kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara za Ikuyufusi –Mkenda,  Kitae-Lituhi KM 84.5, Lituhi –Mbamba Bay KM 112.5 na kukamilisha kwa wakati daraja la Ruhuhu linalounganisha mkoa wa Ruvuma na Njombe kupitia Ludewa ili kurahisisha huduma za usafiri na uchukuzi mkoani Ruvuma.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia), mara baada ya kukagua kivuko cha Mv. Ruhuhu kinachotoa huduma kwa wakazi wa Wilaya za Nyasa na Mbinga mkoani Ruvuma na Ludewa mkoani Njombe.
 Muonekano wa makaa ya mawe katika kijiji cha Ikuyufusi, Serikali imeamua kujenga barabara ya lami kati ya Ikuyufusi na Mkenda ili kuwezesha shughuli za uchukuzi wa rasilimali hiyo mkoani Ruvuma kutekelezeka kikamilifu. 
 Muonekano wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 60 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Ruvuma.
Muonekano wa mtambo wa kusaga kokoto kwaajili ya ujenzi wa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay KM 66 ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaendelea mkoani Ruvuma.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA

yaani makala yote WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/waziri-kamwelwe-ataka-kasi-ujenzi-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAZIRI KAMWELWE ATAKA KASI UJENZI WA BARABARA MKOANI RUVUMA"

Post a Comment

Loading...