Loading...

WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA

Loading...
WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA
link : WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA

soma pia


WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA

Na Felix Mwagara, Mwanza. 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (pichani) , amefiwa na mdogo wake aitwae Josiah Chitage Lugola, aliyekua anaishi jijini Mwanza. Waziri Lugola ambaye ndiye Msemaji wa familia hiyo, alisema mdogo wake Josiah (51) alifariki dunia leo asubuhi Oktoba 7, 2018 na mwili wa marehemu
umehifadhiwa katika Hospitali ya Sekour Toure, jijini Mwanza. 
Waziri Lugola aliongeza kuwa, msiba upo Kijiji cha Nyamitwebili, Kata ya Nyamihyolo, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda Mkoa wa Mara. Waziri Lugola alikua wilayani Bunda kikazi ndipo akapata taarifa hizo za kushtukiza za msiba wa mdogo wake. 
Waziri Lugola alisema msiba huo ni wa ghafla, umeshtua familia na hakika mdogo wake huyo ameacha pengo kubwa katika ukoo wao. 
"Msiba huu ni mkubwa, na pia umetikisa familia yetu, kifo kinapangwa na Mungu, hivyo tunamuombea Mungu, mdogo wangu apokelewe peponi, amina," alisema Waziri Lugola. 
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu, ametoa pole kwa Waziri Lugola pamoja na familia kwa ujumla. 
"Wizara inatoa pole kwa familia ya Waziri Lugola, ndugu wote, jamaa na marafiki kutokana na msiba huo," alisema Kingu.
 Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, taarifa za mazishi zitatolewa baada ya kikao cha familia.


Hivyo makala WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA

yaani makala yote WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/waziri-lugola-afiwa-na-mdogo-wake.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI LUGOLA AFIWA NA MDOGO WAKE, JIJINI MWANZA"

Post a Comment

Loading...