Loading...
title : WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NCHINI
link : WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NCHINI
WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NCHINI
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa Maonesho ya kimataifa ya Utalii ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yatakayofanyika Oktoba 12 hadi 14.
Maonesho hayo yameandaliwa na Bodi ya Utalii Nchini (TTB) yatafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC yakiwa na lengo la kuwaunganisha wafanyabishara wadogo na wa kati wa utalii Tanzania pamoja na wafanyabishara kutoka masoko makuu ya utalii duniani yameweza kudhaminiwa na wadhamini kadhaa wakiongozwa na Tanzania Ocean Cruisng and Safaris Ltd.
Akizungumzia maandalizi kueleka maonesho ya mwaka huu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi amesema kuwa maandalizi yamekaamilika kwa asilimia kubwa na mgeni rasmi akitaraiwa kuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Amesema kuwa, maonesho hayo yatakuwa yanafunguliwa kuanzia saa nne asubuhi nna kufungwa saa 12 jioni na huduma mbalimbali zitakuwa zinafanyika ikiwemo bidhaa za utalii, semina zitakazokuwa zinaendelea ambapo jumla ya mada 24 zitawasilishwa na watalaamu waliobobea kwenye masuala ya utalii.
Devotha amesema kuwa,maonesho yatajumuisha jumla ya mataifa 27 kutoka nje ya Afrika na mataifa 15 ya ndani ya Afrika na zote zitaleta bidhaa zao za utalii na pia kuhudhuriwa na vyombo vya habari 300 duniani.
"Maonesho haya yatahudhuriwa na mataifa 42, mataifa 15 yakiwa ni kutoka Afrika kama vile Uganda, Kenya, Ethiopia, Rwanda, Burundi, Congo, Malawi, Namibia, Zimbabwe, Ghana, Cote D'ivoire, Nigeria, Malawi, Tunisia, Misri na Afrika Kusini huku mataifa mengie 27 kutoka nje ya Afrika nayo yatashiriki wakiwemo Marekani, Canada, Sweden, Italy, Uingereza, Ujerumani, Urusi, Ubelgiji, Australia, India na nchi zingine"amesema Devotha.
Amesema kuwa katika maonesho hayo pia kutakuwa na vyakula vya kiasili vitakavyopikwa hapo hapo na wanafunzi kutoka vyuo vya utalii nchini
ili washiriki na wageni wawezse kufahamu vyakula vya kiutamaduni nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Nchini (TTB) Devotha Mdachi akizungumza na waandishi wa habari maandalizi ya kuelekea maonesho ya kimataifa ya Utalii ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yatakayofanyika Oktoba 12 hadi 14. Kulia ni Meneja Mauzo na Masoko wa Tanzania Ocean Cruising Safaris Christine Jengo na kushoto ni Meneja wa Ukumbi wa Kimataifa wa JNICC Assah Mwambene.
Maandalizi ya mabanda ya maonesho ya Maonesho ya kimataifa ya Utalii ya Swahili International Tourism Expo (SITE) yatakayofanyika Oktoba 12 hadi 14 kwenye ukumbi wa kimataifa wa JNICC
Hivyo makala WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NCHINI
yaani makala yote WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NCHINI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/10/waziri-mkuu-mgeni-rasmi-maonesho-ya.html
0 Response to "WAZIRI MKUU MGENI RASMI MAONESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NCHINI"
Post a Comment