Loading...
title : BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA.
link : BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA.
BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA.
BAADA ya mjadala wa muda mrefu hatimaye Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Tanga limeamua rasmi eneo la Mwakidila lililopo Kata ya Tangasisi kuwa sehemu sahihi ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya Tanga ambao utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.5
Awali hospitali hiyo ilitarajiwa kujengwa katika kata ya Masiwani ambapo tayari jengo la utawala la ghorofa moja lilikwisha jengwa ambalo linadaiwa kugharamia kiasi cha shilingi Milioni 700.Mjadala uliibuka ndani ya kikao hicho cha baraza hilo ambapo madiwani walipingana eneo gani linaweza kuwa sahihi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo mchakato wake unadaiwa kuanza tangu mwaka 2005.
Akizungumza Mwenyekiti wa baraza hilo Mstahiki Meya Mustafa Seleboss alisema kweli yapo maeneo matatu yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo kila eneo linachangamoto zake huku akibainisha umuhimu wa hospitali hiyo kujengwa katika eneo hilo la Mwakidila.Aidha alisema Halmashauri imekwisha pokea kiasi cha shilingi Milioni 500 kati bilini 1.5 toka Serikali kuu kwa awamu ya kwanza ya ujenzi wa hospitali hiyo ambayo itaondoa sitofahamu ya kutokuwepo kwa Hospitali hiyo ndani ya Wilaya.
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza katika kikao hicho
Hivyo makala BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA.
yaani makala yote BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/baraza-la-madiwani-jijini-tanga-laamua.html
0 Response to "BARAZA LA MADIWANI JIJINI TANGA LAAMUA SEHEMU ITAKAPOJENGWA HOSPITALI YA WILAYA."
Post a Comment