Loading...
title : ASILIMIA 13-17 YA WATOTO WOTE WANAOZALIWA NCHINI HUZALIWA NJITI
link : ASILIMIA 13-17 YA WATOTO WOTE WANAOZALIWA NCHINI HUZALIWA NJITI
ASILIMIA 13-17 YA WATOTO WOTE WANAOZALIWA NCHINI HUZALIWA NJITI
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.
CHAMA cha Madaktari bingwa wa watoto nchini kimefanya kongamano lake la kwanza la kisayansi kwa watoto wachanga likiwa na kauli mbiu ya "Kila pumzi ni ya thamani" likiwa na malengo ya kufundisha watumishi wa afya jinsi ya kuwahudumia watoto wachanga ili kupunguza vifo vya watoto walio chini ya mwezi mmoja.
Akifungua kongamano hilo kwa niaba ya Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa. Lawrence Museru amesema kuwa Tanzania inakabiliwa na tatizo kubwa la vifo vya watoto wachanga chini ya mwezi mmoja na asilimia kubwa ya watoto hao huwa ni njiti na takwimu zinaonesha kuwa asilimia 13-17 ya watoto wanaozaliwa nchini huwa njiti.
Amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa ikiripoti programu mbalimbali ambazo lengo lake ni kupunguza vifo vya watoto wachanga na wale walio chini ya miaka 5, programu hizo ni pamoja na zile za kumsaidia mtoto kupumua baada ya kuzaliwa pamoja na kupanua huduma za watoto wachanga kwa kujenga wodi za watoto wachanga katika hospitali za Wilaya na Halmashauri pamoja na kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya kuhusiana na namna ya kuwahudumia watoto wachanga na programu hizo zimesaidia sana katika kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Aidha amesema kuwa kuanzishwa kwa wodi za watoto wachanga itasaidia pia kutatua changamoto ya matibabu kwa watoto hao na maboresho yanayoendelea kufanyika yatasaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga na kuhakikisha watoto wachanga hasa njiti wanapata huduma bora zinazostahili.
Hivyo makala ASILIMIA 13-17 YA WATOTO WOTE WANAOZALIWA NCHINI HUZALIWA NJITI
yaani makala yote ASILIMIA 13-17 YA WATOTO WOTE WANAOZALIWA NCHINI HUZALIWA NJITI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ASILIMIA 13-17 YA WATOTO WOTE WANAOZALIWA NCHINI HUZALIWA NJITI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/asilimia-13-17-ya-watoto-wote.html
0 Response to "ASILIMIA 13-17 YA WATOTO WOTE WANAOZALIWA NCHINI HUZALIWA NJITI"
Post a Comment