Loading...
title : BASATA WASHUSHA RUNGU KWA WCB WAWATOZA FAINI YA MILIONI 9/-
link : BASATA WASHUSHA RUNGU KWA WCB WAWATOZA FAINI YA MILIONI 9/-
BASATA WASHUSHA RUNGU KWA WCB WAWATOZA FAINI YA MILIONI 9/-
Na Khadija Seif,Globu ya jamii .
BARAZA la Sanaa Tanzania(BASATA) limewatoza faini ya Sh.milioni tatu kila mmoja Msanii Raymond Mwakyusa a.k.a Rayvanny na Naseeb Abdull maarufu Diamond pamoja na lebo ya WCB baada ya kukaidi kuufuta wimbo wao wa Mwanza kwenye Youtube.
Kwa mujibu wa BASATA ilitoa tamko kwa wasanii hao wanaotoka lebo la WCB kuufuta wimbo huo jana kabla ya saa 10:30 jioni na kutochezwa redioni na kwenye luninga lakini hawakufanya hivyo.
Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa bado anasisitiza kuondolewa kwa wimbo kwa mujibu wa sheria , kanuni na taratibu za baraza hilo kwani ndio wasimamizi wakuu wa kazi za sanaa nchini .
Mngereza ametoa rai kwa vyombo vyote,mitandao ya kijamii,watu ,pamoja na kumbi za starehe kutotumia wimbo huo kwani umeshafungwa rasmi toka siku ya jana.
Kwa upande wa Meneja wa Lebo hiyo ya WCB Said Fella maarufu kama Mkubwa Fella amesema wamepokea taarifa hizo na kukubaliana nao kuwa ifike pahala wasanii wajue kuwa wamekosea na Basata kama wazazi au walezi wapo kwa ajili ya kurekebisha vijana na kuwalea kwa ujumla na kuwafundisha maadili mazuri kwa mustakabali ya nchini kwa ujumla.
Fella ameeleza kuwa katika kutengeneza burudani lazima kukubaliana na changamoto ili uwe imara, hivyo basi kikao cha kwanza kimeshamalizika wanasubiri kikao kingine baada ya siku tatu.
Hivyo makala BASATA WASHUSHA RUNGU KWA WCB WAWATOZA FAINI YA MILIONI 9/-
yaani makala yote BASATA WASHUSHA RUNGU KWA WCB WAWATOZA FAINI YA MILIONI 9/- Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BASATA WASHUSHA RUNGU KWA WCB WAWATOZA FAINI YA MILIONI 9/- mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/basata-washusha-rungu-kwa-wcb-wawatoza.html
0 Response to "BASATA WASHUSHA RUNGU KWA WCB WAWATOZA FAINI YA MILIONI 9/-"
Post a Comment