Loading...
title : Butiku aitaka VETA kutumia karakana zake kuzalisha bidhaa, kuchonga vipuli
link : Butiku aitaka VETA kutumia karakana zake kuzalisha bidhaa, kuchonga vipuli
Butiku aitaka VETA kutumia karakana zake kuzalisha bidhaa, kuchonga vipuli
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku ameitaka Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kutumia vifaa vilivyopo katika karakana zake kuchonga vipuli na kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa mahitaji mbalimbali nchini.
Butiku alitoa ushauri huo wakati wa mahafali ya chuo cha VETA Dar es Salaam yaliyofanyika Novemba 23, 2018.
Alisema baada ya kutembea kwenye karakana mbalimbali na kuhojiana na walimu na wanafunzi, amebaini kuwa VETA ina rasilimali na hazina kubwa ya mashine na ujuzi wa walimu na wanafunzi ambao ukitumiwa vyema unaweza kuzalisha vitu vingi ambavyo kwa kiasi kikubwa bado vinafanywa na watu binafsi au kununuliwa kutoka nje ya nchi.
“nimejionea vifaa vingi ambavyo naamini vikitumika vizuri vinaweza kuleta manufaa makubwa sana kwa taifa, ifike mahali sasa vifaa mlivyonavyo katika karakana zenu viweze kutengeneza mashine nyingine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ” Alisema
Alitoa mfano wa karakana ya uchapaji ambayo alisema ikiimarishwa inaweza kufanya shughuli nyingi sana za uchapaji wa vitu mbalimbali kwa kuwa ina vifaa na wataalam muhimu vya kuweza kufanya shughuli hizo kwa ufanisi mkubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku akizungumza katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa VETA Dkt Pancras Bujulu akizungumza kuhusiana na mpipango ya VETA katika kutoa ujuzi bobezi katika kupunguza uhaba mafundi katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa waajiri kutoka kampuni ya PLASCO Fidelis Mashauri akitoa maelezo ya mchango wa VETA katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha VETA Dar es Salaam Violeth Fumbo akitoa taarifa katika katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Wahitimu wakionyesha umahiri wao katika katika mahafali ya 48 ya Mafunzo ya Ufundi Stadi Daraja la Pili ya Chuo VETA Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala Butiku aitaka VETA kutumia karakana zake kuzalisha bidhaa, kuchonga vipuli
yaani makala yote Butiku aitaka VETA kutumia karakana zake kuzalisha bidhaa, kuchonga vipuli Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Butiku aitaka VETA kutumia karakana zake kuzalisha bidhaa, kuchonga vipuli mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/butiku-aitaka-veta-kutumia-karakana.html
0 Response to "Butiku aitaka VETA kutumia karakana zake kuzalisha bidhaa, kuchonga vipuli"
Post a Comment