Loading...

OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

Loading...
OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA
link : OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

soma pia


OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA



Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekabidhi kiwanja kwa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ili wakala hiyo ianze ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.

Akikabidhi kiwanja hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Musa Joseph amesema ujenzi wa Ofisi hiyo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais, Dkt John Pombe Magufuli ya kuhamishia shughuli za Serikali Makao Makuu ya nchi Dodoma.

Bw. Joseph amefafanua kuwa, kiwanja kilichokabidhiwa kina ukubwa wa ekari 5.7 na kuwataka TBA kuanza ujenzi mara moja ili kuwawezesha watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwahudumia wananchi wakiwa katika mji wa Serikali.

Bw. Joseph ameongeza kuwa, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora tayari imeshaingiza fedha kwenye Akaunti ya Wakala wa Majengo Tanzania kiasi cha shilingi 700, 000,000/=  ili kuiwezesha TBA kuanza ujenzi na kuongeza kuwa nia ya kufanya malipo mapema ni kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi kwa wakati.

Akipokea kiwanja hicho, Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania mkoani Dodoma, Mhandisi David H. Shunu ameishukuru Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuiamini TBA na kuahidi kukamilisha ujenzi wa ofisi hizo kwa wakati na kwa kiwango bora. 
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph akiwasisitiza Wataalam wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kukamilisha ujenzi wa ofisi kwa wakati katika Mji wa Serikali ili iweze kutumika kuwahudumia wananchi.
002
Afisa Ugavi Mwandamizi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Deograsius Michael (kulia) akikabidhi hati ya makabidhiano ya kiwanja kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Dodoma, Mhandisi David H. Shunu (kushoto) kwa lengo la kuanza ujenzi wa Ofisi katika Mji wa Serikali. Anayeshuhudia ni Afisa Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Benard Makanda.
003
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Musa Joseph (wa pili kushoto) akizungumza na Wataalam  wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) mara baada ya kukabidhi kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi katika Mji wa Serikali uliopo Ihumwa jijini Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>


Hivyo makala OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA

yaani makala yote OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/ofisi-ya-rais-utumishi-yakabidhi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "OFISI YA RAIS-UTUMISHI YAKABIDHI KIWANJA KWA TBA ILI KUANZA UJENZI WA OFISI KATIKA MJI WA SERIKALI JIJINI DODOMA"

Post a Comment

Loading...