Loading...
title : CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI
link : CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI
CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI
Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
SERIKALI ya China kupitia ubalozi wake nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es saalam wameandaa semina maalumu ambayo imelenga kujadili na kubadilishana mawazo kuhusiana na kuimaimarisha masuala ya biashara.
Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo naibu Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Mhandisi Stellah Manyanya amesema kuwa semina hiyo imeandaliwa na Serikali ya China chini ya ubalozi wa nchini kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ajili ya kujenga uhusiano pamoja na kujenga na kuimarisha mahusiano ya kibiashara.
Manyanya amesema kuwa semina hiyo imelenga kupanga mikakati ya kushirikiana baina ya nchi hizo mbili pamoja na faida kwa nchi hizo za Tanzania na China ambazo zimekuwa na uhusiano bora kwa muda mrefu na ameeleza kuwa Tanzania ina rasilimali za kutosha na mahusiano hayo yatasaidia sana katika kufikia malengo ya nchi ya kufikia uchumi wa kati 2025. Amesema kuwa agenda ya viwanda wana malengo ya kuongeza rasimali hasa za kilimo, madini nakadharika.
Pia amesema kuwa semina hiyo ambayo wazawa wanashiriki itakua chachu ya kufungua milango katika sekta ya viwanda. Pia amesema kuwa, "Katika kuwainua wazalishaji (wakulima) tutatoa elimu kuhusiana na masoko na ukuaji wa viwanda nchini na tutahakikisha wanajihusisha na kilimo chenye tija na ninawahakikishia kuwa watanufaika na mikakati inayofuata na kutambua namna ya kufanya kilimo kitakachowasaidia" ameeleza Manyanya.
Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na uwekezaji Mhandisi. Stellah Manyanya akizungumza wakati wa akifungua semina hiyo iliyoshirikisha wadau wa biashara kutoka Tanzania na China.
Balozi wa China nchini Wang Ke akizungumza wakati wa semina hiyo ya kuimarisha uhusiano ambapo amesema kuwa wapo bega kwa bega na serikali ya Tanzania katika kuhakikisha malengo ya kufikia uchumi wa kati 2025 yanafikiwa.
Baadhi wa washiriki wa semina wakifuatilia mjadala huo ambapo wadau mbalimbali wa kiuchumi wamekutana na kubadilishana mawazo juu ya namna bora ya kukuza uchumi.
Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Stellah Manyanya na Balozi wa China nchini Wang ke wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya wadau wa biashara wa hapa nchini na kutoka nchini China.
(Picha na Agnes Francis, Blogu ya Jamii.)
Hivyo makala CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI
yaani makala yote CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/china-na-tanzania-yazidi-kuimairisha.html
0 Response to "CHINA NA TANZANIA YAZIDI KUIMAIRISHA UHUSIANO KUKUZA UCHUMI"
Post a Comment