Loading...
title : DC Mjema awashauri Wazazi kunyonyesha watoto wao wawe na Lishe bora.
link : DC Mjema awashauri Wazazi kunyonyesha watoto wao wawe na Lishe bora.
DC Mjema awashauri Wazazi kunyonyesha watoto wao wawe na Lishe bora.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimkabidhi mkataba wa lishe Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumane Shauri Dar es Salaam leo ,wakati alipokuwa akitiliana saini mkataba huo kwa Wilaya ya Ilala Picha na Heri Shaaban
Na Heri Shaaban
Mwambawahabari
MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewashauri Wazazi Wilayani Ilala kunyonyesha watoto wao ili wawe na lishe bora.
Mjema aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati wa kumsainisha mkataba Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala katika kutekeleza afua za lishe Manispaa Ilala.
"Wazazi nawaomba pindi mnapojifungua wanyonyesheni watoto wenu maziwa mpaka mda ufike msiwakatishe ni halali yao kwa ajili ya afya bora ya mtoto"alisema Mjema.
Aidha pia aliwaka wananchi wake kula mro kamili na vyakula vya zamani kuachana na vyakula vya kisasa.
Alisema katika nchi yetu Tanzania inaitajika Taifa bora lipatikane kwa kuwa na afya bora aliagiza elimu itolewe shuleni,katika nyumba za ibada ili kukabiliana na utapiamlo.
Aidha amewataka wajumbe wa Kamati ya Lishe ndani ya Halmashauri ya Ilala kusimamia na kuakikisha wanapambana na changamoto za lishe duni .
Amewashauri wazazi kuakikisha wanawapa watoto wao haki za msingi katika lishe kina mama wanatakiwa wanawapa watoto wao virutubisho vizuri.
Alisema halmashauri ndio kitovu cha utekelezaji hapa nchini na ili kuweza kukabiliana na utapiamlo inatakiwa tuwe na mikakati na mipango thabiti kwa kutoa rasilimali fedha na watu na kila mdau kuonyesha bayana mchango wake katika kukabiliana na utapia mlo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri amesema upungufu wa lishe mwilini unaweza kuleta madhara mbalimbali amewataka wananchi wa ilala kura mro kamili kwa afya bora.
Mwisho
Hivyo makala DC Mjema awashauri Wazazi kunyonyesha watoto wao wawe na Lishe bora.
yaani makala yote DC Mjema awashauri Wazazi kunyonyesha watoto wao wawe na Lishe bora. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC Mjema awashauri Wazazi kunyonyesha watoto wao wawe na Lishe bora. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/dc-mjema-awashauri-wazazi-kunyonyesha.html
0 Response to "DC Mjema awashauri Wazazi kunyonyesha watoto wao wawe na Lishe bora."
Post a Comment