Loading...

Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi

Loading...
Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi
link : Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi

soma pia


Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi amewataka wafanyakazi wa Taasisi hiyo kufanya kazi kwa bidii huku wakimtanguliza Mungu mbele kwani huduma wanayoitoa inagusa uhai wa watu.

Prof. Janabi ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga maafisa uuguzi wawili ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma na kumpongeza mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha wa Julai-Septemba 2018.

Alisema kazi ya kuwahudumia wagonjwa siyo kazi rahisi sana kuna wakati wagonjwa wanakuwa wakali wao na ndugu zao jambo la muhimu ni kuwa wavumilivu na kuwahudumia kwa moyo wa upendo.

“Leo hii tunawaaga wafanyakazi wenzetu ambao wanastaafu kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma, kazi waliyoifanya ni ngumu wanastahili pongezi. Mmoja amefanya kazi miaka 40 na mwingine miaka 35 katika kipindi chao chote walichokuwa kazini hawakuwahi kushtakiwa kwa utovu wa nidhamu”.

“Jambo la muhimu kwetu sisi tunaobaki tuwaige mfano tujitahidi kuwahi kazini , tuwepo eneo la kazi na kufanya kazi muda wote wa kazi, tushirikiane na tuheshimiane kwa kufanya hivi tutaweza kutoa huduma bora kwa wagonjwa wetu wa moyo”, alisema Prof. Janabi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni moja mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019 Ramadhani Mpili wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu na kumpongeza mfanyakazi bora iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha kutambua utendaji wake wa kazi kwa kipindi chote cha utumishi wa Umma Afisa Muuguzi Mkuu Msaidizi Mstaafu Agnes Mtaki wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu na kumpongeza mfanyakazi bora iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi hiyo hiyo Robert Mallya. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi ngao ya kutambua utendaji wake wa kazi mhudumu wa Afya Mwandamizi Mstaafu Magdalena Masanno wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu na kumpongeza mfanyakazi bora iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Huduma ya Uuguzi wa Taasisi hiyo hiyo Robert Mallya. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na wastaafu Magdalena Masanno na Agnes Mtaki na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo mara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaaga wastaafu hao na kumpongeza mfanyakazi bora iliyofanyika leo katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam. 




Hivyo makala Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi

yaani makala yote Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/fanyeni-kazi-kwa-bidii-huku.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Fanyeni kazi Kwa Bidii Huku Mkimtanguliza Mungu Mbele kwani Huduma Wanayoitoa Inagusa Uhai wa Watu – Prof. Mohamed Janabi"

Post a Comment

Loading...