Loading...

Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020

Loading...
Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020
link : Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020

soma pia


Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020

Na Ripota Wetu, Morogoro

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimesema kupatikana kwa wagombea wa udiwani na ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 kutatokana na kuthibitika kwa vigezo vya ushiriki wao katika shughuli za maendeleo ya chama hicho.

Pia, kimesema hadhi wanaoyopata ama wabunge ambao baadhi yao huteuliwa na kuwa mawaziri au manaibu waziri huku madiwani wakiwa wenyeviti wa halmashauri na mameya ni kutokana na heshima ya CCM kukubalika kwa wananchi.

Hayo yalielezwa jana Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Karogelesi alipokuwa akifunga mafunzo ya siasa, itikadi na maadili kwa vijana wa chama hicho huko Kilosa mkoani Morogoro.Kalogelesi alisema chama ndicho kinachowapa tiketi wanachama wake kugombea ubunge na udiwani hivyo wanapochaguliwa hawapaswi kujiweka mbali na shughuli za ujenzi wa CCM.

Alisema hakuna mwanafunzi anayeweza kujivunia kufanikiwa kwake kielimu ikiwa hawezi kutambua au kuheshimu mchango mkubwa uliotolewa na walimu wake ama katika masomo ya awali au shule ya msingi."Ili tuwapitishe wagombea wetu kwenye udiwani au ubunge mwaka 2020, tutampima kila mgombea kutokana na ushiriki wake katika kazi za chama bila kumtazama usoni. Sifa ya msingi na ya awali nje ya uanachama wake ni kujihusisha kwa kwake na maendeleo ya CCM," alisema Karogelesi.

Mwenyekiti huyo alisema chama cha siasa kitakachokosa kujijenga, kuimarika na kukubalika hakitapata madiwani na wabunge hivyo hata rais atashindwa kuteua mawaziri na manaibu wake pia kwenye majiji na halmashauri hakutakuwa na wenyeviti au mameya wa CCM.

Aliwataka wabunge wa kuchaguguliwa, madiwani na wale wa viti maalumu kutambua kuwa kufika kwao walipo sasa kumetokana na nguvu ya chama na sio uwezo wao binafsi.Kalogeresi aliwataka wanachama wa CCM na jumuiya zake kutambua kuwa wana wajibu na ulazmia wa kuishi kwa kuheshimu misingi ya chama kikatiba, kinidhamu na kimaadili ili kila kiongozi haiba yake iwe ni kioo kinachoakisi mema kwa chama na jamii. 

Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa alimuagiza Katibu wa CCM Mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka, kuwaandikia barua ya ukumbusho wabunge na madiwani wote juu ya ushiriki na wajibu wao ndani ya chama na kwenye jamii.Pia, makatibu wote wa CCM na jumuiya zake mkoani aliwataka kutoa maelekezo na kuwataka wanachama wao kujiweka mbali na vitendo vya udalali wa kisiasa na rushwa.


Hivyo makala Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020

yaani makala yote Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/kalogeresi-atoa-vigezo-vya-kuwapata.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Kalogeresi atoa vigezo vya kuwapata wagombea 2020"

Post a Comment

Loading...