Loading...
title : NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALLU AMEZINDUA HUDUMA YA UMEME WA BEI NAFUU REA JARIBU MPAKANI MKOANI PWANI
link : NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALLU AMEZINDUA HUDUMA YA UMEME WA BEI NAFUU REA JARIBU MPAKANI MKOANI PWANI
NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALLU AMEZINDUA HUDUMA YA UMEME WA BEI NAFUU REA JARIBU MPAKANI MKOANI PWANI
Na Linda Shebby, Pwani
NAIBU Waziri wa Nishati Subira Mgallu amezindua huduma ya usambazaji wa umeme wa vijijini REA katika nyumba 22 za awali katika kijiji cha Jaribu Magharibi kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani ambapo mpango huo umejipanga kuhakikisha inapeleka huduma ya umeme huo wa bei rahisi katika vijiji 7,873 vilivyopo nchini kote.
Alisema kuwa, huduma hiyo ya usambazaji wa umeme Vijijini chini ya REA kwasasa umefikia hatua ya mzunguko wa pili ambapo mpaka sasa tayari Vijiji 235 tayari vimepata umeme na huku mzunguko wa tatu utaanza Machi mwakani.
Mgallu alisema kuwa huduma hiyo ya umeme wa Vijijini inatolewa kwa gharama ya Sh. 27,000 tu kwa kaya moja na kwamba Serikali imeweka kiwango hicho ili kuhakikisha kila Mtanzania anayeishi maeneo ya Vijijini ananufaika na huduma hiyo .
“Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli imejipanga na imeelekeza nguvu zake katika kuhakikisha mnafikiwa na huduma ya umeme popote mlipo ndiyo maana imeweka gharama nafuu ili kusudi kila mwananchi anayeishi Kijijini aweze kumudu gharama na kupata huduma hii ya umeme,”alisema Mgallu.
Alisema kuwa kupatikana kwa huduma hiyo ya umeme Vijijini inachochea maendeleo ambapo aliwaomba wananchi wanaofikiwa na huduma hiyo kuitumia kikamilifu katika kufanya shughuli zao za uzalishaji kupitia biashara zitakazoweza kuwaongezea kipato.
Hatahivyo,Mgallu aliziomba kaya ambazo bado hazijalipia ni vyema zikachangamkia fursa hiyo ili waweze kunufaika na huduma hiyo kwa haraka kwakuwa Serikali imekusudia kupeleka umeme huo kwa kila aina ya nyumba zote iwe ya udongo ama iliyojengwa kisasa zote ziwe na umeme bila ya ubaguzi.
“Serikali itapeleka umeme huu kwa kila nyumba iwe ya Tembe,Udongo au Matofali, hatutobagua nyumba ila cha msingi ni kuhakikisha unaweka miundombinu ya waya vizuri(Wiring) na unalipia kiasi cha Sh .27,000 tu za kuunganishiwa kwahiyo nawaomba mtumie fursa hii kikamilifu,”alisema
Kwa upande wake Mhandisi Mkuu wa Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Pwani Selemani Mgwira,alisema kuwa Mkoa wa Pwani mpaka sasa unajumla ya Vijiji 150 na kwamba jitihada za kusambaza umeme huo bado zinaendelea kama ambavyo Serikali imeweka mipango yake.
Kuhusu Halmashauri ya Kibiti Mgwira alisema kuwa Kibiti inajumla ya Vijiji 19 ambapo kati yake Vijiji vinne tayari vimepata huduma hiyoya umeme wa bei nafuu( REA) na kwamba watahakikisha wanapeleka huduma hiyo katika vijiji vingine na kwamba watahakikisha kila anayehitaji umeme huo anapata huduma haraka.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgallu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Jaribu Magharibi kilichopo katika Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani kuhusiana na usambazaji wa umeme wa vijijini REA huku akiwataka wachangamkie fursa hiyo ili kila nyumba iwake taa za umeme na kuachana na matumizi ya vibatari na mishumaa kwani matumizi hayo yanahatarisha usalama wa mali na maisha yao.
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgallu akibonyeza swichi ya umeme kwenye nguzo akiashiria kuwasha umeme wa REA katika kijiji cha Jaribu Mpakani kilichopo katika Halmashauri ya Kibiti Mkoani Pwani.
Hivyo makala NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALLU AMEZINDUA HUDUMA YA UMEME WA BEI NAFUU REA JARIBU MPAKANI MKOANI PWANI
yaani makala yote NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALLU AMEZINDUA HUDUMA YA UMEME WA BEI NAFUU REA JARIBU MPAKANI MKOANI PWANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALLU AMEZINDUA HUDUMA YA UMEME WA BEI NAFUU REA JARIBU MPAKANI MKOANI PWANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/naibu-waziri-wa-nishati-subira-mgallu.html
0 Response to "NAIBU WAZIRI WA NISHATI SUBIRA MGALLU AMEZINDUA HUDUMA YA UMEME WA BEI NAFUU REA JARIBU MPAKANI MKOANI PWANI"
Post a Comment