Loading...
title : KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU
link : KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU
KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU
NA LUSUNGU HELELA .
Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu amewatoa hofu watumishi wa Taasisi zenye jukumu la kulinda na kuhifadhi Wanyamapori na Misitu nchini kuwa hakuna maslahi yao yatakayobadilika baada ya ujio wa Jeshi Usu
Naibu Waziri Kanyasu ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana na watumishi hao tangu alipoteuliwa kushika wadhifa wa Naibu Waziri katika Wizara hiyo nyeti kwa uchumi wa nchi. Amesema ziara yake imelenga kuzifahamu Taasisi anazoziongoza ili kujua namna zinavyotenda kazi na changamoto zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi.
Akizungumza kuhusu utendaji wa Jeshi USU, Naibu Waziri Kanyasu amesema kufuatia mabadiliko ya mfumo wa utendaji kutoka katika mfumo wa kiraia na kuwa Jeshi USU kutakuwa na mabadiliko kiutendaji yatakayoendana na taratibu za Jeshi USU lakini utakaoheshimu na kulinda maslahi ya watumishi.
Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa, uanzishwaji wa Jeshi hilo haukusudii kubadili maslahi ya watumishi hao na endapo maslahi hayo yatabadilika basi yatakuwa na mabadiliko chanya kwao. Naibu Waziri Kanyasu ameongeza kuwa Jeshi USU litaongeza nidhamu uwajibikaji na maadili kwa watumishi wa sekta ya Maliasili na Utalii ili waweze kusimamia ipasavyo uhifadhi endelevu wa maliasili na si vinginevyo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (wa pili kushoto) akimsikiliza Mhifadhi ,kuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya enoe la n Ngorongoro, Dkt.Freddy Manongi wakati alipowatembelea jana katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( kushoto) akipewa maelezo na Dkt. Maurus Msuha (katikati) wakiwa kwenye sehemu ya kuonea wanyamapori (View point) ya Ngorongoro Kreta wakati alipotembelea jana kwa ajili ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu ( wa kwanza kushoto) akiwa ameongozana na Menejimenti ya Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro akipewa maelezo wakati alipotembelea jana kabla ya kuzungumza na kuwasikiliza watumishi wa Mamlaka hiyo juu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi
Watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu wakati alipowatembelea jana.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa na baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro wakiamungalia Faru mwenye umri wa miaka 65 ambaye ni faru mzee duniani .
Hivyo makala KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU
yaani makala yote KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/kanyasu-awatoa-hofu-watumishi-juu-ya.html
0 Response to "KANYASU AWATOA HOFU WATUMISHI JUU YA MASLAHI YAO BAADA YA UJIO WA JESHI USU"
Post a Comment