Loading...
title : MAHAKAMA YAELEZWA UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA AKRAM AZIZI HAUJAKAMILIKA
link : MAHAKAMA YAELEZWA UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA AKRAM AZIZI HAUJAKAMILIKA
MAHAKAMA YAELEZWA UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA AKRAM AZIZI HAUJAKAMILIKA
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Akram Azizi ambaye ni mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi bado haujakamilika.
Wakili wa Serikali Elia Athanas ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa."Mheshimiwa keai hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, tunaimba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa" amedai wakili Athanas.
Kufuatia malezo hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 26 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.Katika kesi hiyo, Mshtakiwa Azizi anakabiliwa na mashtaka 75 yakiwemo mashtaka 71 ya kukutwa na Silaha za aina mbali mbali mbali, utakatishaji wa fedha kiasi cha USD 9018.
Pia anakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh milioni 108, risasi 6496 na pia anakabiliwa na kosa la kukutwa na nyama ya Nyati, Kilogramu 65 yenye thamani ya Shilingi Mil 4.35 bila kuwa na kibali, ambalo anadaiwa kulitenda Oktoba 30,2018 huko Oysterbay Kinondoni Dar es Salaam.
Katika shtaka la utakatishaji mshtakiwa anadaiwa, kati ya Juni 2018 na Oktoba 30. 2018 katika eneo la Osterbay, alijipatia jumla ya USD 9018 huku akijua kuwa kiasi hicho cha fedha ni zao la kosa tangulizi la kujihusisha na biashara haramu ya nyara za serikali pamoja na kukutwa na silaha bila kibali.
Katika mashtaka ya kukutwa na risasi mshtakiwa anadaiwa, Oktoba 30. 2018 (Jana) huko Osterbay, alikutwa na risasi 4092 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa kibali cha silaha.
Pia Imedaiwa Oktoba 31.2018 (leo) huko huko Osterbay mshtakiwa alikutwa na risasi 2404 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa mrajisi wa silaha.
Mfanyabiashara Akram Azizi ambaye ni mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi akiwasili leo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi yake ya uhujumu uchumi inayomkabili .
Hivyo makala MAHAKAMA YAELEZWA UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA AKRAM AZIZI HAUJAKAMILIKA
yaani makala yote MAHAKAMA YAELEZWA UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA AKRAM AZIZI HAUJAKAMILIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAELEZWA UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA AKRAM AZIZI HAUJAKAMILIKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/mahakama-yaelezwa-upelelezi-kesi-ya.html
0 Response to "MAHAKAMA YAELEZWA UPELELEZI KESI YA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MFANYABIASHARA AKRAM AZIZI HAUJAKAMILIKA"
Post a Comment