Loading...

MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO

Loading...
MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO
link : MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO

soma pia


MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Watumishi wa Serikali Wilayani Rombo kufanya kazi kwa kushirikiana.

Makamu wa Rais ameyasema hayo jana  mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya hiyo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya Mhe. Agnes Hokororo.

“Wote tunajenga nyumba inayoitwa Tanzania katika nafasi yako yoyote ulipo unajenga nyumba inayitwa Tanzania, kwa itikadi yako yoyote uliyonayo unajenga nyumba inayoitwa Tanzania tunatawaliwa na sheria moja, tunataliwa na miongozo hiyo hiyo ya Serikali, kanuni na mambo mengine na hiyo hiyo Serikali”.

Katika ziara yake Wilayani Rombo Makamu wa Rais alikagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Rombo, mradi wa maji Shimbi Mashariki,kukagua shamba la Miti Rongai.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo pia alipata nafasi ya kuwasalimu wananchi wa Tarakea waliojitokeza barabarani kumsalimia na alihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Keni-Mengeni.

Kwa upande mwingine Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa Serikali hii inafanya jambo la kihistoria kwa kukamilisha ujenzi wa vituo vya Afya 350.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungungumza na Watumishi wa Wilaya ya Rombo mara baada ya kupokea taarifa ya Wilaya hiyo. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
2 4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya mradi wa ujenzi wa jengo la Utawala la Halmashauri ya Rombo kutoka kwa Mhandisi wa Halmashauri Mhandisi Boniface Vedasto. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
5 6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wananchi wa Tarakea waliojitokeza kumsalimia wakati alipokuwa njiani kuelekea kwenye shamba la miti Rongai. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua kitalu cha miche wakati alipotembelea shamba la miti la Serikali lililopo Rongai Rombo. Makamu wa Rais yupo kwenye ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Kilimanjaro. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). 


Hivyo makala MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO

yaani makala yote MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/makamu-wa-rais-aendelea-na-ziara.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MAKAMU WA RAIS AENDELEA NA ZIARA WILAYANI ROMBO"

Post a Comment

Loading...