Loading...
title : MASHIBA- UPATIKANAJI WA ARDHI NA BAADHI YA VIBALI NI TATIZO KWA BAADHI YA WAWEKEZAJI
link : MASHIBA- UPATIKANAJI WA ARDHI NA BAADHI YA VIBALI NI TATIZO KWA BAADHI YA WAWEKEZAJI
MASHIBA- UPATIKANAJI WA ARDHI NA BAADHI YA VIBALI NI TATIZO KWA BAADHI YA WAWEKEZAJI
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MENEJA wa kanda ya Mashariki wa kituo cha uwekezaji Tanzania TIC Venance Mashiba , asema lipo tatizo kwa baadhi ya wawekezaji hasa katika upatikanaji wa ardhi na baadhi ya vibali vinavyochukua muda mrefu kwenye upatikanaji wake .
Alisema hayo wakati akizungumzia changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ,wakati wa maonyesho ya bidhaa za viwandani yanayoendelea Pichandege Kibaha ,mkoani Pwani .
Mashiba alieleza ,huduma za uwekezaji ni mtambuka ambapo zinatolewa na taasisi mbalimbali ambazo taratibu zake zikigongana inasababisha changamoto ya ucheleweshaji wa huduma kwa wawekezaji."Tatizo kubwa lipo kwenye ardhi kwani ardhi zote zipo chini ya halmashauri ,mwekezaji lazima apeleke wazo lake halmashauri na akipatiwa ardhi ndipo aje kwetu kuandikisha mradi wake "
"Sasa mradi wake utakubaliwa endapo atapata ardhi na taratibu za upatikanaji wa ardhi ni nyingi na ni ndefu"alifafanua Mashiba .Mashiba alisema ,kutokana na hilo kituo hicho , kimeimarisha huduma zake kwa kuongeza taasisi 11 za serikali ambazo zinatoa huduma mbalimbali, vibali na leseni ili mwekezaji apate huduma mahala pamoja na sio kuzunguka .
Alisema, ikitokea mwekezaji ana changamoto zinazohusuana na huduma zinazotolewa kwenye hizo taasisi basi wakuu wa taasisi hizo hukutana na kuamua kuzitatua .Nae mkuu wa Mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo aliipongeza TIC kwa jitihada zake katika kukuza na kuvutia uwekezaji nchini na namna inavyohudumia wawekezaji kupitia huduma za mahala pamoja zinazotolewa na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya ofisi za kituo hicho .
Alielezea kwamba ,Mkoa huo ni miongoni mwa mikoa inayopokea wawekezaji na hivyo nguvu ya kuwahudumia iimarishwe. Ndikilo aliitaka TIC kuhakikisha inapata taarifa zinazohusiana na uwekezaji Mkoani humo kwa kuwasiliana na halmashauri za mkoa ."Kwa kufanya hivyo kutarahisisha uratibu na huduma kwa wawekezaji wa Mkoa na Taifa kijumla " alisema Ndikilo.
Alisisitiza ni vyema wakawa na taarifa za maeneo ya uwekezaji yaliyotengwa pamoja na ,takwimu za miradi ya uwekezaji.Katika kuhakikisha mkoa wa Pwani unaendelea kuvutia wawekezaji Ndikilo alisema atawasilisha TIC maeneo ambayo tayari yametengwa kwa ajili hiyo ili yatafutiwe wawekezaji.
Mkuu wa mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo (kushoto )akizungumza wakati alipotembelea banda la maonyesho ya ,kituo cha uwekezaji Tanzania( TIC )katika maonyesho ya bidhaa za viwandani Pichandege ,Kibaha Pwani.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Hivyo makala MASHIBA- UPATIKANAJI WA ARDHI NA BAADHI YA VIBALI NI TATIZO KWA BAADHI YA WAWEKEZAJI
yaani makala yote MASHIBA- UPATIKANAJI WA ARDHI NA BAADHI YA VIBALI NI TATIZO KWA BAADHI YA WAWEKEZAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MASHIBA- UPATIKANAJI WA ARDHI NA BAADHI YA VIBALI NI TATIZO KWA BAADHI YA WAWEKEZAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/mashiba-upatikanaji-wa-ardhi-na-baadhi.html
0 Response to "MASHIBA- UPATIKANAJI WA ARDHI NA BAADHI YA VIBALI NI TATIZO KWA BAADHI YA WAWEKEZAJI"
Post a Comment