Loading...
title : MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI
link : MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI
MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Joseph Nyamhanga, ameagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), kumuandikia barua mkandarasi wa Kampuni ya Impesa di Construzioni anayejenga kituo cha ukaguzi wa pamoja (one stop inspection station) eneo la Manyoni mkoani Singida na Nyakanazi mkoani Kagera kurejea eneo la kazi na kuendelea na ujenzi.
Akizungumza katika kijiji cha Muhalala mkoani Singida wakati wa ukaguzi wa kituo hicho, Katibu Mkuu huyo amesema Serikali tayari imeshashughulikia madai ya mkandarasi huyo, hivyo hana sababu ya kutoendelea na ujenzi wa mradi huo. "Naagiza Mkandarasi huyu arudi eneo lake la kazi na kuanza kazi ya ujenzi wa mradi huu mara moja", amesema Mhandisi Nyamhanga.
Aidha, Mhandisi Nyamhanga, ameeleza kuwa jumla ya gharama za mradi wa vituo hivyo ni takribani shilingi bilioni 55, ambayo itahusisha gharama za ujenzi, usimamizi na fidia. Mhandisi Nyamhanga amefafanua kuwa ujenzi wa kituo hicho unaenda sambamba na ujenzi wa kituo kingine eneo la Nyakanazi mkoani Kagera ambapo kituo kingine cha vigwaza mkoani Pwani kimeshakamilika na hivyo kutafanya jumla ya vituo vikuu vitatu vya ukaguzi vyenye umbali wa kilomita 500 kutoka kwa kila kimoja.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Singida Mhandisi Masige Matari, akitoa taarifa ya mradi kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja (One Stop Inspection Station), katika kijiji cha Muhalala, wilayani Manyoni, mkoani humo.
Muonekano wa baadhi ya nyumba za watumishi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Polisi watakaoishi mara baada ya ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Pamoja kukamilika katika kijiji cha Muhalala, Wilayani Manyoni, Mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri Adel alkhateeb, anayesimamia ujenzi wa barabara wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati alipoukagua mradi huo, Mkoani Tabora.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akikagua moja ya boksi kalvati iliyojengwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, akikagua moja ya boksi kalvati iliyojengwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chaya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami, Mkoani Tabora.
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Tabora Mhandisi Damian Ndabalinze, akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), kuhusu hatua zilizofikiwa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyahua-Chanya yenye urefu wa KM 85.4 kwa kiwango cha lami wakati Katibu huyo alipokagua mradi huo, mkoani Tabora.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI
yaani makala yote MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/mhandisi-nyamhanga-aagiza-mkandarasi_28.html
0 Response to "MHANDISI NYAMHANGA AAGIZA MKANDARASI KURUDI ENEO LA KAZI"
Post a Comment