Loading...

Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo.

Loading...
Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo.
link : Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo.

soma pia


Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo.


Mwambawahabari
Na Heri Shaaban
MKURUGENZI wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri awataka Wenyeviti wa Serikali ya Mitaa wa Manispaa ya Ilala na Watendaji wa Mitaa kusimamia mikopo ya serikali iweze kufika kwa walengwa .


Mkurugenzi wa Ilala aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya utaratibu mpya wa utoaji mikopo kwa wanawake ,Vijana,na Watu wenye Ulemavu .


Shauri alisema mikopo hiyo inatolewa na Serikali aina riba kwa wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu  ili iweze kuwafikia wananchi kama ilivyokusudiwa  na  atakayepitisha majina yake kwa udanganyifu atachukuliwa hatua.

"Tumetoa elimu hii ya mafunzo ya utaratibu wa utoaji mikopo ngazi ya mitaa kwa sababu ndio mmebeba dhamana kwa wananchi wenu na mkopo huo ugaiwe kwa wakazi wa Manispaa ya Ilala mwananchi ajulikane anapoishi" alisema Shauri.

Alisema Serikali ya awamu ya tano inaongozwa na Rais John Magufuli anatetea Wanyonge imeelekeza halmashauri zote  nchini kuendelea kutenga fedha na kuanza kutoa mikopo hiyo ya kuendeleza wanawake,Vijana,na watu wenye ulemavu bila riba.


Aidha alisema mafunzo hayo yajadili kwa kina kubainisha njia sahii za  kuwabaini walengwa halisi wa mfuko katika maeneo yao wanayotoka Pia Watumishi watakaokuika kwa makusudi hatua zitachukuliwa dhidi yao  kwa kupelekea hasara au kutoa mikopo kwa wasiostaili.

Aliwataka Wenyeviti  wa Serikali ya Mitaa na Watendaji wa mitaa waweke mpango madhubuti itakayoonyesha namna watakavyotoa elimu juu ya mfuko huo wa wananchi wa Wilaya ya Ilala,


Kwa upande mwingine Mkurugenzi Shauri aliwataka wananchi watakaochukua mkopo huo wajiunge na Bima ya Afya TIKA ili iweze kuwasaidia katika majanga mbalimbali ikiwemo kuumwa.

Kwa upande wake Ofisa      
Ofisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Ilala Fransica Makoye alisema shilingi milioni 670 zimetengwa kwa mwaka wa fedha 2018  /2019 kwa ajili ya utoaji wa mikopo isiyo na riba kwa wananchi wa wilaya ya Ilala .


Makoye alisema dhumuni la mafunzo ya kukamilisha mchakato wa utoaji  mikopo ya ngazi kata Wenyeviti na Watendaji tumewapa elimu kwa ajili ya kuwajengea uelewa wa sababu wapo karibuni na wananchi na mikopo yote inapitia kwao.

Alisema dhumuni mikopo hiyo kuwafikia Wajasiriamali 15000 wa Wilaya ya Ilala pia kuna vikundi vipya vitapata mikopo hiyo changamoto wakopaji wengi sio waminifu katika malejesho hivyo amewataka wakope na kulejesha ili wengine waweze kunufaika na mikopo hiyo ya serikali kwani mikopo kwa manufaa yao wasichukulie kitu cha kupita.

Wakati huohuo Makoye alieleza Taasisi isiyo ya Kiserikali  GURU PLANET ambayo ipo manispaa ya Ilala , iliomba kufanya kazi ya kuwasaidia Wajasiriamali kupata masoko ya bidhaa zao Halmashauri ya Ilala inamtambua ilimpatia kibali cha kufanya kazi ndani ya manispaa ya Ilala bila kuchangisha fedha Wananchi .



Hivyo makala Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo.

yaani makala yote Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/mkurugenzi-ilala-awataka-wenyeviti.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mkurugenzi Ilala awataka Wenyeviti Watendaji kusimamia mikopo."

Post a Comment

Loading...