Loading...
title : MKUTANO MKUU APHFTA WAWAKUTANISHA WADAU, SUALA LA ADA NA USAJILI LATOLEWA MAJIBU
link : MKUTANO MKUU APHFTA WAWAKUTANISHA WADAU, SUALA LA ADA NA USAJILI LATOLEWA MAJIBU
MKUTANO MKUU APHFTA WAWAKUTANISHA WADAU, SUALA LA ADA NA USAJILI LATOLEWA MAJIBU
Leandra Gabriel na Karama Kenyunko Blogu ya jamii
SERIKALI imesema ipo katika mpango wa kutengeneza muongozo ambao utasaidia katika utoaji huduma kwenye hospitali binafsi ikiwemo suala la ongezeko la gharama ambazo zinawafanya wananchi wa kawaida kushindwa kupata huduma.
Mkurugenzi wa tiba kutoka Wizara ya Afya, maendeleo ya jamii, jinsia wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima amesema hayo leo Novemba 20.2018 wakati wa uzinduzi wa mkutano wa 19 wa wadau wa afya na hospitali binafsi. Amesema kuwa muongozo huo utasaidia hospitali binafsi ambazo hutoa huduma kwa gharama kubwa kuacha kuwabagua wagonjwa wa dharula kwani ni lazima afya ya mtu ije kwanza.
"Tunashughulikana hospitali zenye tozo kubwa kwa wagonjwa, kwani ni sawa kwao kuweka gharama zao kutokana na mfumo wa kutibu magonjwa maalumu, ni sawa kwa hospitali hizo kuwa na gharama zao ila kwa magonjwa ya dharura lazima huduma zitolewe bila kuangalia hadhi ya hospitali hizo" ameeleza Dkt. Gwajima.
Aidha amesema kuwa malengo ya kufanya mkutano huo ni kujadili juu ya kuimarisha utoaji wa huduma katika vituo vyao vya kutolea huduma. Dkt. Gwajima amesema kuwa sekta binafsi zinamiliki asilimia 40 za utoaji wa huduma za afya nchini na pia wanashiriki sana katika utoaji ajira na wao kama serikali wanatambua mchango wao na changamoto zao lazima wazifanyie kazi.
Mwenyekiti wa chama cha wamiliki binafsi wa vituo vya afya nchini (APHFTA) Dkt. Kaushik Ramaiya (kushoto) wakifuatilia mjadala uliozinduliwa na Mkurugenzi wa tiba leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Afisa mtendaji wa APHFTA Dkt. Samwel Ogillo. (Picha na Erick Picson, Blogu ya jamii)
Mkurugenzi wa tiba kutoka Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati akifungua mkutano wa 19 wa wanachama na wamiliki binafsi wa vituo vya afya leo jijini Dar es Salaam.
Afisa mtendaji wa wanachama wa wamiliki binafsi wa vituo vya afya Dkt. Samwel Ogillo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo ambao umejikita zaidi katika kujadili namna ya kuimarisha zaidi sekta ya afya nchini .
Afisa mtendaji wa wanachama wa wamiliki binafsi wa vituo vya afya Dkt. Samwel Ogillo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mkutano huo ambao umejikita zaidi katika kujadili namna ya kuimarisha zaidi sekta ya afya nchini .
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MKUTANO MKUU APHFTA WAWAKUTANISHA WADAU, SUALA LA ADA NA USAJILI LATOLEWA MAJIBU
yaani makala yote MKUTANO MKUU APHFTA WAWAKUTANISHA WADAU, SUALA LA ADA NA USAJILI LATOLEWA MAJIBU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKUTANO MKUU APHFTA WAWAKUTANISHA WADAU, SUALA LA ADA NA USAJILI LATOLEWA MAJIBU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/mkutano-mkuu-aphfta-wawakutanisha-wadau.html
0 Response to "MKUTANO MKUU APHFTA WAWAKUTANISHA WADAU, SUALA LA ADA NA USAJILI LATOLEWA MAJIBU"
Post a Comment