Loading...

TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO

Loading...
TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO
link : TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO

soma pia


TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA)imewataka wale wote wenye kuuza bidhaa za mawasiliano ikiwemo simu za mkononi,Radio na Runinga kuhakikisha wanajisajili kwao ili wananchi wapate huduma zilizo sahihi.

Akizungumza kwenye semina ya huduma za utangazaji kwa channeli zinazotazamwa bila malipo Meneja wa mamlaka hiyo Mhandisi Fransis Msungu amesema kuwa hapa Arusha mamlaka hiyo imebaini kuwa wafanyabiashara wengi wana leseni za biashara lakini za mamlaka hiyo wengi wao hawana.

Amesema kuwa maswali mengi yalioelekezwa kwa mamlaka hiyo imeonyesha mafundi wa simu na maduka mengi hayana leseni za mamlaka hiyo hivyo kutoa wito kwao kuangalia na kujisajili haraka kwao ili kuweza kumlinda mlaji.

“Nawasihi wote kuhakikisha wanajisajili haraka kwao ili kuwezakuondoa malalamiko yanayotolewa na walaji kwa mamlaka yetu utaona hapa Arusha kuna maduka 40 yenye leseni zetu mengi yaliopo bado hayajasajiliwa sanjari na mafundi wa simu”alitanabaisha Msungu.Kwa Upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Arusha David Mwakiposa amesema kuwa mbali na malalamiko mbali mbali yaliotolewa na washiriki wa mkutano huo suala zima ni mashirikiano kati ya Tcra na wadau mbalimbali na semina hiyo imefungua milango kwa wananchi kwani elimu itawafikia walengwa ambao ni wananchi.

Amesema kuwa semina hiyo inatakiwa kuwa endelevu na watendaji wamejipanga kuhakikisha kuwafikishia wananchi kwenye maeneo yao na tutarajie kuondoa changamoto mbali mbali zinazo wakabili wananchi hususani ya wizi wa mtandao.“Natoa rai kwa TCRA kuhakikisha changamoto mbali mbali zinazoelekezwa kwao kuzitafutia ufumbuzi ili kuondoa kero na adha wanayokutana nayo wananchi katika maeneo mbali mbali hapa nchini tunashukuru sana sisi tumepata uelewa wa masuala haya ya channel zisizolipiwa na tunaahidi kutoa elimu kwa wananchi”alisema Mwakiposa

Aidha Baadhi ya washiriki mbali mbali walioshiriki katika semina hiyo wamepata uelewa ila wakaitaka Tcra kuenda mbele zaidi katika suala zima la utoaji wa elimu kwa wananchi sanjari na kutatua changamoto mbali mbali wanazokutana nazo walaji wa mamalaka hiyo.


Hivyo makala TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO

yaani makala yote TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/tcra-yawataka-wauza-runinga-na-mafundi_21.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TCRA YAWATAKA WAUZA RUNINGA NA MAFUNDI SIMU KUJISAJILI KWENYE MAMLAKA HIYO"

Post a Comment

Loading...