Loading...
title : NAIBU MEYA WA MANISPAA YA ILALA AKUTANA NA WALEMAVU KATA YA VINGUNGUTI,AWAPA MIKAKATI MIZITO.
link : NAIBU MEYA WA MANISPAA YA ILALA AKUTANA NA WALEMAVU KATA YA VINGUNGUTI,AWAPA MIKAKATI MIZITO.
NAIBU MEYA WA MANISPAA YA ILALA AKUTANA NA WALEMAVU KATA YA VINGUNGUTI,AWAPA MIKAKATI MIZITO.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omari kumbilamoto, akizungumza na walemavu wa kata ya Vingunguti katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mashujaa(Picha zote na John Luhende)
Na John Luhende
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa kata ya Vingunguti Omari kumbilamoto, amekutana na walevu wa kata hiyo kwalengo la kuwapa elimu kuhusu fursa za kiuchumi, zinazotolewa na Manispaa ya Ilala ikiwemo mikopo ya asilimia mbili ambayo inatolewa na halmashauri hiyo.
Akizungumza katika mkutano huo Kumbilamoto, amewataka walemavu hao kujitokeza kwa wingi kuchukua mikopo ya walemavu inayotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ili waweze kujiendeleza kibiashara kwa na kuacha utegemezi kwa kuwa wanao uwezo wa kufanya kazi.
“Fedha zenu zipo Halmashauri na nimezungumza katika Baraza la madiwani, ninyi mpewe kipaumbele,nimedhamiria kuwa saidia nataka niwaambie ninyi mna weza wala msijisikie wanyonyonge na Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inawajailisana na wasaidizi wake hatutawaacha pekeyenu” alisema.
Aidha amewahamasisha kujiunga katika umoja wao ili iwe rahisi kusaidiwa wanapo hitaji msaada kutoka kwa wadau mbambali, watakao saidia mfuko wao ili waweze kusaidiana katika matatizo madogo madogo.
“Pia nivema mkawa na umoja wenu ambao mtakuwa mna saidiana mnakuwa na Accout Bank , ambayo mtakuwa mnachangiwa fedha zitakazo wasidia hatammoja wenu akiumwa mnaweza kusaidia kwa matibabu”alisema
Kumbilamoto pia amechangia fedha walemavu hao kwaajili ya kufungua Account Bank ya CRDB, na pesa ya usajili wa umoja wao ili waweze kutambulika na serikali ,na ameahidi kuhamasisha watu mbali mbali kuwachangia walemavu hao .
“Nitajitahidi kuhamasisha na kuongea na Marafiki zangu walioko ughaibuni ili wanisaidie kuwachangia msipate shida maana kwa sasa hapa mlipo hata mtu akiumwa homa ya shilingi 5000 mtaanza kuomba omba kwa mjomba shagazi lakini mkiwa na fedha yenu itawasaidia”alisema
Kwaupande wao baadhi ya walemavu waliopata fursa ya kutoa mawazo yao katika mkutano huo wamemuomba Naibu meya Kumbilamoto kuwatafutia eneo ambalo watafanya biashara zao katika masoko.
“Mstahiki Meya tunaomba sana kiongozi utusaidie sisi walemavu tupatiwe nafasi katika Masoko yanayo jengwa mfano soko la kisutu na Buguruni hataka kama hatutapata wote hata baadhi yetu na wengine katika masoko menginea yaliyoko Manispaa ya Ilala”alisema Sikujua Mbwembwe.
Naye Omary Ramadhani ,aliomba walemavu watengewe eneo maalumu ili wawe wanauza bidhaa zao kwa rejareja na jumla ili waweze kurahisisha ulipaji wa mikopo.
Katibu wa umoja wa walemavu kata ya vingunguti John Damasi, akizungumza katika mkutano .
Baadhi ya walemavu waliofika katika mkutano wa Naibu meya wakisikiliza kwa makini maezeo kutoka kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omari Kumbilamoto.
Baadhi ya walemavu waliofika katika mkutano wa Naibu meya wakisikiliza kwa makini maezeo kutoka kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omari Kumbilamoto.
Baadhi ya walemavu waliofika katika mkutano wa Naibu meya wakisikiliza kwa makini maezeo kutoka kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omari Kumbilamoto.
Hivyo makala NAIBU MEYA WA MANISPAA YA ILALA AKUTANA NA WALEMAVU KATA YA VINGUNGUTI,AWAPA MIKAKATI MIZITO.
yaani makala yote NAIBU MEYA WA MANISPAA YA ILALA AKUTANA NA WALEMAVU KATA YA VINGUNGUTI,AWAPA MIKAKATI MIZITO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NAIBU MEYA WA MANISPAA YA ILALA AKUTANA NA WALEMAVU KATA YA VINGUNGUTI,AWAPA MIKAKATI MIZITO. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/naibu-meya-wa-manispaa-ya-ilala-akutana.html
0 Response to "NAIBU MEYA WA MANISPAA YA ILALA AKUTANA NA WALEMAVU KATA YA VINGUNGUTI,AWAPA MIKAKATI MIZITO."
Post a Comment