Loading...

Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani

Loading...
Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani
link : Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani

soma pia


Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani

Na Teresia Mhagama

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani ameeleza kuwa ukomo wa kuunganishia umeme wateja walioomba kuunganishiwa huduma hiyo kwa muda mrefu ni Agosti 30, 2017 na Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) atakayeshindwa kutimiza agizo hilo atashushwa cheo.

Dkt. Kalemani aliyasema hayo kwa nyakati tofauti akiwa katika ziara ya kuzindua mradi wa Usambazaji Umeme Vijijini wa Awamu ya Tatu katika mikoa ya Rukwa, Ruvuma na Mtwara.

"Unakuta kuna wateja wameomba kuunganishiwa umeme miezi kadhaa iliyopita lakini mpaka sasa hawajaunganishwa wakati vifaa vipo, kwa hili lazima tuchukue hatua kwa Meneja kama ni wa wilaya, mkoa, Kanda au Mkurugenzi atayechelewa kuunganishia wateja Umeme," alisema Dkt. Kalemani.

Dkt. Kalemani alisema kuwa muda wa kumuunganishia mteja Umeme mara anapolipia huduma hiyo ni Siku Saba na si vinginevyo."Natambua kuna maeneo ambayo TANESCO mnafanya kazi vizuri lakini katika hili tutawajibishana," alisisitiza Dkt. Kalemani.

Wakati huohuo. Dkt. Kalemani aliwaagiza watendaji wa TANESCO kuhakikisha kuwa watu wote wanaofanya kazi ya kutandaza nyaya za umeme ndani ya nyumba wawe wanatambulika na Shirika hilo ili kuondoa tatizo la vishoka kufanya kazi hiyo pasipo ufanisi na baadaye kuleta madhafa kama ya moto.

Vilevile aliwataka watendaji hao kutokukaa maofisini na badala yake wawafuate wananchi sehemu walipo, suala ambalo litafanya Shirika hilo kuongeza idadi ya wateja na kuwaondolea wananchi kero ya kutembea kwa umbali mrefu kufuata huduma TANESCO.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika mkoa wa Ruvuma.



Hivyo makala Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani

yaani makala yote Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2017/08/ukomo-wa-kushughulikia-maombi-ya-muda.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Ukomo wa kushughulikia maombi ya muda mrefu ya kuunganisha Umeme ni Agosti 30- Dkt Kalemani"

Post a Comment

Loading...