Loading...

Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini

Loading...
Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini
link : Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini

soma pia


Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini


Naibu Waziri Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya leo amefanya mazungumzo na balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Sahabu Isah kuhusu mambo mbalimbali ya uwekezaji nchini.

Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ofisi ndogo za wizara hiyo Jijini Dar-es-salaam, Naibu Waziri Manyanaya na mgeni wake wamezungumza masuala mbalimbali ya uwekezaji ikiwemo uwekezaji wa uliofanywa na kampuni ya kuzalisha saruji ya Dangote.

“Tumefurahi kumuona balozi amekuja kututembelea na kufuatilia masuala ya uwekezaji yanayohusu nchi yake”. Amesisitiza Mhe. Manyanya. Mhe. Manyanya ameeleza kuwa kupitia kikao hicho wameweza kubalishana uzoefu katika masuala ya maendeleo ya nchi zote mbili.

Mhe. Waziri amemuhakikishia balozi huyo wa Nigeria kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi ya Nigeria katika masuala ya Uwekezaji na pia wizara yake iko tayari muda wowote kumokea endapo atakutana na changamoto yeyote. Mbali ya kumhakikishia uhsirikiano, mheshimiwa Manyanya pia alitoa shukran za serikali kwa uwekezaji uliofanywa na nchi ya Nigeria “sisi tunafurahi kumuona Dangote amewekeza, na tungependa uwekezaji wake uendelee ili watanzania waendelee kufaidika na uwekezaji huo”, aliongeza mhandisi Manyanya.

Kwa upande wake Mhe. Sahabu amehaidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina na nchi hizo mbili na amefurahishwa na hatua za serikali za kutatua changamoto za wafanyabiashara mbalimbali kutoka Nigeria waliowekeza nchini.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya kwenye kikao na balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Sahabu Isah alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dar-es-salaam. Mhandisi Manyanya na mgeni wake wamezungumza mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Kushoto (suti ya blu) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Joseph Bchweishaija. 
Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Stella Manyanya, kwenye picha ya pamoja na balozi wa Nigeria nchini Tanzania, Mhe. Sahabu Isah baada ya kumaliza mazungumzo yaliohusu uwekezaji wa nchi ya Nigeria nchini. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Joseph Bchweishaija. 


Hivyo makala Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini

yaani makala yote Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/naibu-waziri-manyanya-akutana-na-balozi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Naibu Waziri Manyanya Akutana Na Balozi Wa Nigeria Nchini"

Post a Comment

Loading...