Loading...

Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi

Loading...
Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi
link : Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi

soma pia


Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi


Na Grace Semfuko-MAELEZO
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mwita Waitara amewataka wafanyabiashara na wenye Viwanda nchini kulipa kodi ya maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufanya miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo itasaidia wananchi wengi.
Waitara alisema ili Serikali iweze kuongeza ufanisi katika kuhudumia jamii wafanyabiashara na wawekezaji katika maenneo mbalimbali wanapaswa kulipa kodi ya mapato ambayo pamoja na kusaidia uongezwaji wa miradi ya maendeleo pia itaboresha mazingira ya biashara na uwekezaji Nchini.
Naibu Waziri Waitara aliyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa Mwaka wa kuelekea katika kilele cha miaka 30 tangu kunzishwa kwa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA uliofanyika Jijini Dar Es Salaam ambapo alisema chama hicho ki mekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha uchumi wa Taifa na kuunga mkono Seikali ya awamu ya tano ya Rais Magufuli inayosisitiza uchumi wa Viwanda
“Wafanyabiashara Lipeni Kodi ya maendeleo, Kodi ndio itatufanya kuwawekea mazingira mazuri ya uwezeshaji na hatimaye mfanye biashara zenu kwa ufanisi mkubwa, sisi tutaendelea kuwawezesha kwani chama chenu ni muhimu sana katika kukuza ustawi wa kijamii” alisema Mwita Waitara Naibu Waziri TAMISEMI.
Nae Kaimu Rais wa Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Kilimo Bw. Octavian Mshiu amsema kwa muda wa miaka 30 Serikali imekuwa ikifanya juhudi za kuhakikisha wawekezaji waliopo katika chama hicho wanaongeza shughuli zao na kusababisha mafanikio makubwa.
Alisema katika Serikali ya awamu ya tano ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa wanachama wake wa kuanzisha viwanda na kufungua biashara kubwa na hivyo kuiomba Serikali kuzidi kuwashauri kwenye masuala mbalimbali ya kuwekeza ili kufikia uchumi wa kati.
TCCIA pia imefungua matawi yake katika Nchi za China na Uturuki ili kupanua shughuli zake na kuwawezesha Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda kufanya biashara zao kimataifa zaidi ambapo Mkurugenzi wa Chamber ya China Bw. Martin Rajabu alisema wanapata ushirikiano mkubwa katika suala zima la kibiashara na raia wa nchini humo.

Chama hicho cha Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda kilianzishwa rasmi mwaka 1988 ambapo kwa mwaka huu kinatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake na miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana na kuwaunganisha wafanyabiashara kimataifa,kuwajengea uwezo,kukuza mitaji yao na kuwawezesha kuimarisha viwanda,biashara na kilimo.


Hivyo makala Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi

yaani makala yote Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/naibu-waziri-tamisemi-awataka.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Naibu Waziri TAMISEMI awataka Wafanyabiashara Kulipa Kodi"

Post a Comment

Loading...