Loading...

Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65

Loading...
Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65
link : Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65

soma pia


Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65

Na Mwandishi Wetu
Serikali imedhamiria kujenga Vituo vya Polisi 65 katika wilaya mbalimbali nchini ikiwa ni juhudi za kukabiliana  na uchakavu na upungufu wa vituo vya polisi nchini.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kutembelea na kukagua Kituo cha Polisi cha Songe ambacho ndio kituo kikuu katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga
Alisema Serikali inatambua changamoto za vituo vya polisi ikiwemo uchakavu, udogo wa majengo katika vituo mbalimbali nchini na iko katika mpango wa kujenga vituo vya polisi 65 ili kuwepo na ulinzi thabiti wa raia na mali zao.
“Serikali inatambua changamoto ya vituo vya polisi hasa katika wilaya mpya nchini, ikiwepo uchakavu wa majengo, kwahiyo uko mkakati maalumu wa kujenga vituo vya polisi 65 nchi nzima ili kuweza kukabiliana na matukio ya kiuhalifu, lengo la serikali ni kuhakikisha raia wake na mali zao zinakua salama na matukio ya kiuhalifu yanapungua na kutoweka kabisa,” alisema Masauni
Alisema Serikali pia inakaribisha nguvu za wananchi na wadau mbalimbali ambao wako tayari kusaidia ujenzi wa vituo vya polisi huku akipongeza baadhi ya maeneo nchini ambako vituo vya polisi vimejengwa kwa ushirikiano wa michango ya wananchi na serikali.
 Naibu  Waziri  wa Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi,  Mhandisi  Hamad  Masauni, akiwaongoza  Wajumbe  wa  Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  kuingia  Kituo  cha  Polisi  cha  Songe, ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  Naibu  Waziri  kukagua  shughuli  za  ulinzi  na  usalama  wilayani  Kilindi  mkoani Tanga .Picha  na  Wizara  ya Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi 
 Naibu  Waziri  wa Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi,  Mhandisi  Hamad  Masauni, akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha  Wajumbe  wa  Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  Naibu  Waziri  kukagua  shughuli  za  ulinzi  na  usalama  wilayani  Kilindi  mkoani Tanga . Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo na Kulia ni Katibu  Tawala  wa  Wilaya  hiyo,  Warda  Abeid.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sauda Mtondoo  akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha  Wajumbe  wa  Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  Naibu  Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) kukagua  shughuli  za  ulinzi  na  usalama  wilayani  Kilindi  mkoani Tanga . Kulia ni  Katibu  Tawala  wa  Wilaya  hiyo, Warda  Abeid.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi , Edward Bukombe, akizungumza katika kikao cha ndani kilichohusisha  Wajumbe  wa  Kamati  ya  Ulinzi  na  Usalama  ya  Wilaya  ya Kilindi  ikiwa  ni ziara  ya  kikazi  ya  Naibu  Waziri  wa  Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani, ) kukagua  shughuli  za  ulinzi  na  usalama  wilayani  Kilindi  mkoani Tanga . Picha  na  Wizara  ya Mambo  ya  Ndani  ya  Nchi

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65

yaani makala yote Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/serikali-kujenga-vituo-vya-polisi-65.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Serikali kujenga Vituo vya Polisi 65"

Post a Comment

Loading...