Loading...

NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI

Loading...
NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI
link : NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI

soma pia


NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI


BENKI ya NMB imetoa msaada wa vitanda tisa vya wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Kigamboni vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni tano. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia kwa wajawazito, vimekabidhiwa leo kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija.

Akikabidhi vitanda hivyo, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wa kawaida wa NMB kurejesha faida kidogo kwa jamii. Alisema Benki hiyo, hutenga takribani bilioni moja fedha ambayo hurejesha kwa jamii kwa kusaidia sekta za afya, elimu na masuala mengine yanayoikumba jamii kama maafa na majanga.

Alisema Benki ya NMB inaunga mkono juhudia za Serikali za kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo afya kwa wananchi, ili jamii ambao ni sehemu ya wateja wa benki hiyo wawe na afya njema."..Kama tunavyojua afya ni huduma ya msingi kwa jamii wakiwemo wateja wetu, hivyo tuna kila sababu ya kuisaidia pale tunapopata fursa ya kufanya hivyo," alisema Bw. Badru Idd katika hotuba yake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija akipokea msaada huo aliipongeza Benki ya NMB kwa juhudi zake za kuendelea kusaaidia sekta mbalimbali za huduma za kijamii. Aliziomba taasisi nyingine kuiga mfano wa Benki ya NMB kutoa sehemu ya faida yake kusaidia jamii ili kuchochea maendeleo ya taifa. Alisema Serikali inapambana katika kuhakikisha inaboresha huduma za afya kwa wananchi, lakini haiwezi kufanikiwa kwa kiwango kikubwa bila kushirikiana na wadau wengine kama ilivyofanya NMB kutoa msaada kwenye kituo hicho cha afya.

Naye Mganga Mfawidhi Kituo cha Afya Kigamboni, Dk. Julius Nyakazilibe alisema msaada wa NMB umefika wakati muafaka kwani kwa sasa kituo kinapanua huduma zake ikiwemo kuongeza majengo hivyo vitasaidia kuziba mapengo yanayojitokeza.

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (wa pili kulia) akimkabidhi sehemu ya msaada wa vitanda vya wagonjwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija (wa pili kushoto) vilivyotolewa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia ni viongozi wa NMB. 
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Bw. Ng'wilebuzu Lubigija akimshukuru meneja wa NMB Tawi la Kigamboni mara baada ya kupokea msaada huo wa vitanda. 
Sehemu ya vitanda vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Kituo cha Afya cha Kigamboni jijini Dar es Salaam. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia wajawazito vinathamani ya shilingi milioni tano. 
Sehemu ya viongozi wa Kituo cha Afya cha Kigamboni cha jijini Dar es Salaam wakifurahiaa sehemu ya msaada pamoja na viongozi wa NMB waaliokabidhi msaada huo. Vitanda hivyo sita (6) vikiwa vya wagonjwa wa kawaida na vitatu (3) vikiwa maalum kwa ajili ya kujifungulia wajawazito vinathamani ya shilingi milioni tano


Hivyo makala NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI

yaani makala yote NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/nmb-yasaidia-vitanda-9-kituo-cha-afya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "NMB YASAIDIA VITANDA 9 KITUO CHA AFYA KIGAMBONI"

Post a Comment

Loading...