Loading...
title : SERIKALI YAFUNGUA FURSA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA
link : SERIKALI YAFUNGUA FURSA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA
SERIKALI YAFUNGUA FURSA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
SERIKALI imesema kuwa katika kukabiliana na uhifadhi mazingira ni wakati muafaka kwa wadau kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko mbadala ambayo haina madhara katika utunzaji wa mazingira.
Akizungumza katika kikao kilichohusisha wadau wa mazingira kuhusu fursa za uwekezaji katika uzalishaji wa mifuko mbadala, Naibu katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Balozi Joseph Edward Sokoine amesema kuwa malengo ya kikao hicho ni kujadili mabadiliko katika uhifadhi ya mazingira pamoja na kujadiliana na wadau juu ya namna bora ya kutokomeza matumizi ya mifuko ya plastiki kwa kutengeneza mifuko mbadala ya karatasi au nguo
Balozi Sokoine amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wajasiriamali kuwekeza katika uzalishaji wa mifuko ya karatasi na nguo ili kuchangia katika uhifadhi wa mazingira na kuongeza kipato chao na kipato ha taifa kwa ujumla.
Balozi Sokoine amesema kauli mbiu ya "Mifuko mbadala kwa ustawi wa afya, mazingira na uchumi wetu" itumike katika kuhamasisha namna bora ya utunzaji wa mazingira kwa jamii kwa ujumla.
Balozi Sokoine amesema kuwa mifuko mbadala iwe na gharama nafuu na amewataka wadau wa mazingira kuendeleza kampeni ya kutokomeza matumizi ya mifuko na plastiki ambayo inachangia katika uchafuzi wa mazingira.
Kwa upande wake Mhandisi kutoka Wizara ya Viwanda, Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais Julius Enock amesema kuwa athari za mifuko ya plastiki ni kubwa sana na hudumu kwa muda mrefu zaidi.
Amesema kuwa takribani mifuko bilioni 7.8 hadi 10 hutumika kwa mwaka nchini na mifuko hiyo hudumu ardhini kwa miaka 500 hadi 1000 huku ikiendelea kuathiri mazingira.
Amesema kuwa mifuko iliyozalishwa 1950 kwa mara ya kwanza bado ipo ardhini ikiendelea kuathiri mazingira kwa kiasi kikubwa huku akitaja athari nyingine ikiwa ni pamoja na kuathiri shughuli za kitalii, kuuwa mifugo na viumbe vya baharini hali ambayo hupelekea kuathiri kipato cha mtu mmoja mmoja na Serikali kwa ujumla.
Julius amesema kuwa asilimia 60 hadi 80 ya taka za plastiki huishia baharini na mkakati wa kutokomeza janga hili ni kwakila mtu kutimiza wajibu wake katika ulinzi wa mazingira .
Hivyo makala SERIKALI YAFUNGUA FURSA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA
yaani makala yote SERIKALI YAFUNGUA FURSA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAFUNGUA FURSA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/serikali-yafungua-fursa-uzalishaji-wa.html
0 Response to "SERIKALI YAFUNGUA FURSA UZALISHAJI WA MIFUKO MBADALA"
Post a Comment