Loading...

SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA

Loading...
SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA
link : SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA

soma pia


SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amerasimisha bandari bubu nne mkoani Tanga kati ya bandari bubu 48 zilizopo mkoani humo wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu hizo na kupata taarifa ya utendaji kazi wa bandari ya Tanga. Nditiye amerasimisha bandari bubu ya Moa iliyopo Wilayani Mkinga, Kigombe (Muheza), Kipumbwi na Mkwaja zilizopo wilayani Pangani.

Nditiye amesema kuwa amerasimisha bandari bubu hizo nne tu kati ya bandari bubu 48 zilizopo mkoani Tanga kwa kuwa zipo mbali na bandari ya Tanga, zipo mipakani na nchi za jirani, kusogeza huduma karibu na wananchi na kuiwezesha Serikali kukusanya tozo na kodi mbali mbali kwa ajli ya kutoa huduma kwa wananchi. 

“Naiagiza TPA kuhakikisha kuwa bandari bubu nne nilizorasimisha zinafanya kazi ifikapo mwishoni mwa mwezi Januari mwaka 2019 na wahakikishe kuwa watumishi wa TPA na TRA wanakuwepo kwenye bandari hizo pamoja na ofisi zote za Serikali zinazohitajika ikwemo Jeshi la Polisi,”.

Pia ameitaka TPA kwa kushirikiana na TRA itoe elimu kwa wateja kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ya Serikali kwa kuwa kiwango cha kodi kinachotozwa ni kidogo ukilinganisha na athari wanazopata wananchi na wafanyabiashara kwa kuhatarisha maisha yao kwa kukwepa kodi na kutumia bandari bubu kupitisha mizigo na bidhaa nje ya bandari rasmi zilizopo na kupita maporini. 

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipokea shukrani za Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Moa, Rambazo A. Mohamedi (wa kwanza kushoto) kwa kurasimisha bandari bubu ya Moa kuwa bandari rasmi. Wa pili kushoto ni Mkuu wa bandari ya Tanga, Percival Salama

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akipokea taarifa ya utendaji kazi wa Bandari ya Tanga kutoka kwa Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama (aliyesimama katikati) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua bandari hiyo

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kulia) akisikiliza kwa makini maelezo kuhusu upakuaji wa mafuta melini kutoka kwa Nahodha Andrew Matilya wakati wa ziara yake ya kukagua bandari ya Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akipokea taarifa kuhusu bandari bubu ya Moa kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Yona Mark wakati wa ziara yake ya kukagua bandari bubu mkoani Tanga. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Bandari ya Tanga, Percival Salama.



Hivyo makala SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA

yaani makala yote SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/serikali-yarasimisha-bandari-bubu-nne.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YARASIMISHA BANDARI BUBU NNE MKOANI TANGA"

Post a Comment

Loading...