Loading...

SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA

Loading...
SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA
link : SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA

soma pia


SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA


Na.Alex Sonna wa Fullshangweblog,Dodoma

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) Jijini Dodoma,wametakiwa kutilia mkazo ulipaji wa mafao ya wastaafu kwa wakati.

Akitoa maagizo hayo leo jijini hapa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde, alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.

Mhe.Mavunde amesema kuwa inatakiwa mlipe kwa wakati mafao kama ilivyo kauli mbiu yenu ya “Tunalipa Kuanzia jana” ili lengo la serikali la kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii, litimie .''Inatakiwa wastaafu wapewe umuhimu wa elimu kabla ya kuwalipa mafao ili waweze kujiandaa vyema kwa kuanzisha miradi na kutunza kumbukumbu za matumizi ya fedha''amesema Mavunde

Aidha Mhe.Mavunde amewaagiza wafanyakazi wote kuhakikisha wanatoa huduma stahiki zenye ubora na kwa wakati ili kuisaidia serikali kusonga mbele katika huduma ya hifadhi ya jamii.“Matarajio ni kwamba mtatoa huduma kwa ufanisi na kwa ubora ili yale matarajio ya serikali yaweze kutimia, awali kulikuwa na malalamiko watu hawapati huduma stahiki lakini naimani hakutakuwa na malalamiko hayo,”amesema Mavunde

Kwa Upande wake, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Dodoma, Meshack Bandawe, amesema kuwa ofisi hiyo imeanza kufanya kazi zake Septemba mosi mwaka huu na kuna wanachama wanaochangia ni zaidi ya laki moja.“Tumejipanga kuwahudumia ipasavyo na hadi sasa tumekusanya Sh.Milioni 880 katika mkoa wa Dodoma na tutaendelea kusimamia na kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria,”amesema Bandawe

Hata hivyo amebainisha kuwa hadi sasa wanachama 2792 wameshapita kupata huduma na wamepokea madai 796 ya wanachama wa mifuko mbalimbali iliyounganishwa kwenye mfuko huo. Bandawe amesema kuwa madai 717 yameshughulikiwa na wanachama wamelipwa mafao yao na mengine 79 yapo kwenye hatua mbalimbali za kufanyiwa kazi katika mkoa wa Dodoma tu.

Aidha amesema takribani wastaafu 1027 wanatarajiwa kustaafu katika kipindi cha 2018/19 ambapo mfuko huo umejipanga kutoa elimu ya kujipanga na ustaafu wao ikiwemo kubuni miradi ya kujiimarisha kiuchumi kwa mkoa wa Dodoma peke yake.
 Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akizungumza waandishi wa habari (hawapo pichani) alipotembelea ofisi za mfuko huo leo jijini Dodoma kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akizungumza na Meneja wa PSSSF Mkoa wa Dodoma, Meshack Bandawe, alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenyeulemavu, Anthony Mavunde,akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa PSSSF Mkoa wa Dodoma leo alipotembelea ofisi za mfuko huo kusikiliza maoni ya wanachama na wadau wanaohudumiwa na PSSSF.


Hivyo makala SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA

yaani makala yote SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/serikali-yaridhishwa-na-huduma-za-psssf.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "SERIKALI YARIDHISHWA NA HUDUMA ZA PSSSF MKOA WA DODOMA"

Post a Comment

Loading...