Loading...

TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza

Loading...
TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza
link : TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza

soma pia


TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza


Mchumi mwandamizi wa Mwanza, Kaswalala Elisha anashikiliwa na Takukuru mkoani hapa kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh300, 000 kutoka kwa mfanyabiashara.

Kwa kawaida Takukuru hutoa taarifa za watu wanaowashikilia kufanya makosa muda mfupi kabla ya kupelekwa mahakamani, lakini naibu mkuu wa Takukuru mkoa, Emmanuel Stenga alizungumzia suala la ofisa huyo wa Serikali bila ya kueleza atafikishwa mahakamani lini.

Stenga aliwaambia waandishi wa habari jijini Mwanza leo kuwa mtuhumiwa huyo alishirikiana na mtu mwingine kutenda kosa hilo Novemba 16, akiwa katika ofisi yake iliyopo katika majengo ya ofisi ya mkuu wa mkoa.

Alisema siku moja kabla ya kunaswa kwenye mtego uliowekwa na maofisa wa Takukuru, mtuhumiwa huyo pamoja na mwenzake ambaye bado anatafutwa walikuwa wakiwasiliana kwa njia ya simu na mfanyabiashara huyo anayejihusisha na uuzaji wa vifaa vya maabara (jina linahifadhiwa) aliyefikisha taarifa Takukuru.

“Pamoja na mambo mengine, watuhumiwa walimtuhumu mfanyabiashara huyo kukwepa kodi na kuiuzia Serikali bidhaa feki na hivyo kumtaka kutoa Sh5 milioni ili asichukuliwe hatua za kisheria,” amesema Stenga

Amesema kosa hilo ni kinyume cha kifungu cha 15 cha Sheria ya Takukuru ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.


Hivyo makala TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza

yaani makala yote TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/takukuru-yamtia-mbaroni-mchumi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TAKUKURU Yamtia Mbaroni Mchumi mwandamizi Jijini Mwanza"

Post a Comment

Loading...