Loading...

TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini

Loading...
TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini
link : TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini

soma pia


TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini



Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini imedhamiria kuendelea kuwajengea uwezo wajasiriamali nchini ili waweze kuzalisha na kukuza biashara zao na kuchangia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda. 

Akizungumza leo Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valley Mutakyamirwa amesema kuwa dhamira yao ni kuendelea kujenga uwezo kwa wajasiriamali hao ili waweze kuchangika katika kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuweka mikakati ya pamoja kati ya wanachama wa Taasisi hiyo. 

“ Wajasiriamali hawa ni wanachama wetu hivyo jukumu letu ni kuhakikisha kuwa tunashirikiana nao katika kuibua changamoto na kuweka mikakati ya pamoja ambayo tunashirikiana na Serikali katika kuona namna bora yakuzitatua “; Alisisistiza Mutakyamirwa 

Akifafanua amesema kuwa, Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali ikiwemo kujenga miundombinu, kupunguza kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kutoka asilimia 20 hadi 18 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya Serikali kuendelea kuimarisha mazingira ya wajasiriamali kufanya biashara. Aliongeza kuwa Warsha hiyo inawasaidia wajasiriamali hao kufanya tathmini ya shughuli wanazofanya na kuja na mikakati ya pamoja itakayoasaidia katika kuimarisha Biashara hapa nchini. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bw. Valency Mutakyamirwa akizungumza na washiriki wa warsha ya siku mbili kuhusu uwezeshaji wa wanachama wa Taasisi hiyo leo Jijini Dodoma ikilenga kuibua changamoto na kuweka mikakati ya pamoja yakuzitatua. 
Meneja Mradi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) Bi. Veneranda Sumila akisisitiza kuhusu umuhimu wa semina ya kuwajengea uwezo wanachama wa TPSF leo Jijini Dodoma wakati wa hafla yakufungua warsha hiyo. 
Mratibu kutoka Taasisi ya Best Dialogue Bi. Manka Kway akizungumzia umuhimu wa Maktaba ya Mtandaoni inayoleta pamoja taarifa za wajasiriamali wa Tanzania ikiwemo tafifi mbalimbali zinazofanyika zikilenga kuchangia katika kukuza biashara hapa nchini. 
Muwezeshaji wa masuala ya Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Patrokil Kanje akizungumzia namna wajasiriamali wa Tanzania wanavyoweza kukuza na kuendeleza biashara zao kwa kutumia mbinu za kisasa wakati wa warsha ya wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi. 
Katibu Mtendaji wa Umoja wa Wachimbaji wa Madini na Nishati Tanzania (TCME) Bw. Gerald Mturi akizungumzia umuhimu wa semina hiyo kwa wanachama wa Taasisi ya Sekta Binafsi. 



Hivyo makala TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini

yaani makala yote TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/tpsf-yadhamiria-kuendelea-kuwezesha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TPSF Yadhamiria Kuendelea Kuwezesha Wajasiriamali Nchini"

Post a Comment

Loading...