Loading...

Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36

Loading...
Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36
link : Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36

soma pia


Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36

Mwambawahabari

Na Grace Semfuko-MAELEZO

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Masanja Kadogosa amesema ujenzi wa Reli ya kisasa ya Standard Gauge (SGR)inayoanzia jijini Dar es Salaam hadi Mwanza unaoendelea nchini umefikia asilimia 36 kwa awamu ya kwanza inayotokea Dar es Salaam hadi Makutupora
Reli hiyo ya Kisasa ya umeme yenye kilomita 336 za njia kuu na kilometa 86 za kupishana treni itakuwa na uwezo wa kwenda kwa mwendo kasi wa kilometa 160 kwa saa na kusafirisha mizigo tani milioni 17 kwa mwaka.

Akizungumza mara baada ya kuwapokea wanafunzi wa vyuo vikuu wanaosomea fani ya uhandisi mitambo na ujenzi waliotembelea mradi huo wa SGR, Kadogosa alisema ipo haja ya vijana wa kike wengi kusomea masomo ya sayansi ili kuongeza wataalamu wengi wa uendeshaji wa Reli hiyo.

“Nafurahi kuona wasichana mnajiingiza katika fani hii ya uhandisi, hii ni fani nzuri na naomba wasichana wengine wasome masomo ya Sayansi ili kuongeza wataalamu wa kuendesha Reli yetu hasa wataalamu wa kike” alisema Kadogosa

Kwa upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) Mhandisi Patrick Barozi alisema bodi hiyo ina wahandisi 23,416 waliosajiliwa ambapo kati yao wahandisi wa kike ni 2,401 sawa na asilimia 10 na kwamba juhudi za dhati za kuwahamasisha kupenda masomo ya kihandisi zinafanyika.

Alisema katika tathmini yao ya miaka 30 iliyopita tangu kuanzishwa kwa bodi ya ERB,wamebaini kuwa wanandisi wa kike wanafanya vizuri katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo na kwamba wamekuwa na uaminifu mkubwa.

“Wahandisi wa kike wanafanya vizuri katika kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi, hapa hatuangalii jinsia tunaangalia kazi lakini wanaposimama wanawake kazi inakwenda vizuri. Sisemi kwamba wanaume wanafanya vibaya, hapana wanafanya kazi nzuri.Kwa kuwa tunazungumzia wanawake basi niseme tu kwamba wanafanya kazi nzuri,” alisema Kaimu Msajili wa Bodi ya ERB Mhandisi Patrick Barozi.

Wakati huo huo Meneja wa Mradi wa Ujenzi wa SGR kipande cha Dar es Salaam –Morogoro, Mhandisi Machibya Masanja alisema kazi ya uenzi wa reli hiyo ya kisasa inaendelea vizuri ambapo kazi kubwa hivi sasa ni ujenzi wa madaraja makubwa ambao umefikia asilimia 46 katika kipande cha kwanza kwenye awamu ya kwanza ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.


Alisema kazi ya utandikaji wa reli kwa kipande cha kwanza ilishaanza na hatua iliyopo sasa ni ya kusawazisha kwenye baadhi ya maeneo inayopita reli hiyo na kujenga madaraja kazi ambayo inaendelea kwa kasi sana.


Hivyo makala Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36

yaani makala yote Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/11/ujenzi-wa-standard-gauge-yafikia.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Ujenzi wa Standard Gauge yafikia asilimia 36"

Post a Comment

Loading...